Polisi wa Kenya wabainisha mshukiwa wa shambulio la kanisa.

Mei 07, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Polisi wa Kenya wamemtambua mshukiwa katika shambulio la kombora la tarehe 29 Aprili katika kanisa huko Nairobi kuwa ni wakala wa al-Shabaab.

Mshambuliaji, ambaye kwa jina la lakabu anajiita “Amar” alikuwa Kismayo, Somalia mwaka uliopita lakini alirudi Kenya mapema mwaka huu, Kamishina wa Polisi Matthew Iteere alisema.

Polisi wametoa picha ya mshukiwa huyo na kutoa wito kwa mtu yeyote mwenye ufahamu ambao utasaidia kukamata kwake kuwezekana, “Ni muhimu kuzingatia kuwa ni mtu hatari na anayeaminika kuwa na silaha aina ya bastola na inawezekana kuwa na mlipuko,” Redio Capital FM ya Kenya ilimnukuu Iteere akisema.

Shambulio hilo Kanisa la Kimataifa la Nyumba ya Miujiza ya Mungu katika eneo la Ngara lilimuua mtu mmoja papo hapo na kujeruhi 15.

Iteere alisema kiongozi wa al-Shabaab huko Kismayo “alidai kuhusika na shambulio hilo na akaapa kufanya mashambulio zaidi ya mabomu ya kujitoa muhanga kwa Kenya”.

Nairobi imeshuhudia mashambulio kadhaa ya mabomu katika maeneo ya raia tangu mwisho wa mwaka 2011, ambapo mlipuko ulioua watu tisa katika kituo cha basi mwezi Machi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 3)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • kerry
    June 14, 2012 @ 06:16:37AM

    Wakenya wengi wasio na hatia wameteseka kutokana na mashambulizi ya al-Shabaab, kwa hivyo wahalifu kama hao lazima wakamatwe na kushughulikiwa ipasavyo, na wale watakaoonekana na makosa wahukumiwe kifo.

  • tumo benjamin
    May 8, 2012 @ 10:01:41AM

    Ajira za serikali zinawezekana kwa kupunguza ajira zinazosababisha vijana kujiunga na kikundi cha kigaidi ili waweze kuishi na kujikimu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo