Kenya kuufanya mtaala wa shule za sekondari kuwa katika mfumo wa dijitali

Mei 04, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Serikali ya Kenya ilitangaza hapo Alhamisi (tarehe 3 Mei) kuingia ubia na kampuni ya LG Electronics, Intel na Microsoft ili kuufanya mtaala wa shule za sekondari kuwa katika mfumo wa dijitali nchini kote.

Kuanzia mwezi ujao, wanafunzi wataweza kupata maandishi ya shule katika mfumo wa dijitali kwa kutumia kompyuta na simu zao za mikononi, ili kuimarisha njia za ufundishaji na usomaji, gazeti la Kenya la Daily Nation liliripoti.

Vitabu na muhtasari ni miongoni mwa vitu vitakavyokuwa katika mfumo wa dijitali, na walimu watapata mafunzo juu ya matumizi ya nyanja hizi mpya.

“Kujifunza kwa njia ya elektroniki (E-learning) kunawarahisishia wanaojifunza na walimu kufahamu dhana na kunaimarisha kiwango cha ufahamu na uwezo wa kujifunza kwa faida ya wanafunzi,” alisema Lydia Nzomo, mkurugenzi wa Taasisi Rasmi ya Elimu Kenya.

Kampuni za LG, Intel na Microsoft zitatoa msaada wa kompyuta kwa shule za Kenya ili kuhakikisha wanafunzi wanaweza kupata machapisho hayo katika mfumo wa dijitali.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo