Maafisa wa Somalia waonya juu ya ukataji miti

Mei 04, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kamishna wa wilaya ya Beled Hawo ameonya dhidi ya ukataji haramu wa miti kwa ajili ya mkaa, na kutangaza faini ya dola 60 kwa watakaovunja amri hiyo, Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti hapo Alhamisi (tarehe 3 Mei).

Naye Mkuu wa Wilaya Mohamoud Ahmed Odweyne, pia hakimu wa wilaya, aliuambia mkusanyiko wa watu katika mji wa mpakani kuwa utawala wa Sunna wal Jamaa utachukua hatua kali kwa yeyote atakayekamatwa akikata miti kwa dhamira ya kutengeneza mkaa kwa kujipatia faida.

Ukataji miti una athari zisizorejesheka kwa mazingira na kunaweza kupelekea njaa, shirika hilo la habari liliripoti.

Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio la kupiga marufuku usafirishaji wa mkaa kutoka Somalia. Asilimia 80 ya mkaa unaozalishwa nchini Somalia unasafirishwa nje, hasa kwenda nchi za Ghuba.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo