Somalia yaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani

Mei 04, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wawakilishi kutoka vyombo vya habari vya Somalia, Chama cha Taifa cha Waandishi wa Habari Wasomali na Wizara ya Habari walitoa taarifa rasmi ya pamoja Alhamisi (tarehe 3 Mei) kuadhimisha Siku ya Vyombo vya Habari Duniani, ambapo walikubaliana kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari.

Kufuatia mkutano kati ya waandishi wa habari na wawakilishi wa wizara, pande mbili ziliamua kwamba “vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuimarisha amani na kuhimiza kuheshimu utawala wa sheria, hasa katika kipindi hiki kigumu cha utawala wa mpito.”

Chama pia kiliitaka serikali kutoa ulinzi zaidi kwa waandishi wa habari. Wanahabari watano wameuawa nchini Somalia mwaka huu, na mauaji ya hivi karibuni ni Jumatano huko Galkayo.

Mwakilishi Maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Balozi Boubacar Gaoussou Diarra aliwapongeza waandishi wa habari wa Somalia kwa nafasi yao muhimu katika kutangaza amani. “Inatia moyo kujua kiwango kikubwa cha bidii na shauku inayoonyeshwa na waandishi wa habari nchini Somalia licha ya mazingira ya hatari wanayofanyia kazi,” alisema katika taarifa yake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alionyesha kuchukizwa na kuongezeka kwa idadi ya waandishi wa habari wanaouawa wakati wakifanya kazi yao.

"Kinga ya kutoshitakiwa kwa wale wanaowashambulia au kuwatishia waandishi wa habari linabakia kuwa tatizo linaloongezeka; ikiwa ni pamoja na mashambulizi yanayofanywa mchana, yakitoa ujumbe wa kikatili sana,” Ban alisema katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo