Umoja wa Mataifa: Maelfu ya watoto wa Kisomali hatarini kufa kwa njaa

Mei 03, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeonya kwamba limepokea asilimia 12 tu kati ya lengo lake lililojiwekea la dola milioni 298 kwa ajili ya kazi za misaada ya kibinaadamu nchini Somalia mwaka huu, ambako kunawaweka maelfu ya watoto wa Kisomali katika hatari ya kufa njaa.

“Kazi hii inaendelea na ni operesheni kubwa sana inayoyaokoa maisha ya watoto kila siku,” alisema msemaji wa UNICEF Marixie Mercado. “Ikiwa hatukupata fedha, programu zetu zote zitapaswa kukatwa,” alisema. “Wale waliokosa chakula kwa kiwango kikubwa ndio walio wenye hatari ya kifo.”

Mercado alisema kiasi cha watoto 325,000 waliokosa chakula cha kutosha wako kwenye uhitaji mkubwa wa msaada.

Alisema ukosefu wa usalama umekuwa kikwazo katika kuwasaidia watoto wenye mahitaji. “Tuna watoto milioni 1.9 ambao hawajafikiwa na chanjo katika maeneo ya kusini na kati kwa sababu ya vikwazo vya kiusalama,” alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • tryphone
    May 4, 2012 @ 03:44:41PM

    Maelezo mazuri, yanajieleza yenyewe.

  • أبراهيم محسن
    May 4, 2012 @ 10:48:13AM

    Al-Shabaab ni kikundi cha kifisadi na kinachotesa watu. Hawawezei daima kujihesabu kuwa ni mujahidina na inatosha kuona wanayakataza mashirika ya misaada ya Kiislamu yaliyokuwa yanaingia eneo lao. Wanataka watu wafe kwa njaa, jambo linalothibitisha kuwa hawana ubinadamu wala hawana hisia, au fikra. Hatusemi lolote bali tunategemea msaada wa Mungu kutusaidia dhidi yao, kwa sababu wamezichafua akili za vijana na kuwafanya waharibu nyumba yao kwa mikono yao wenyewe.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo