Mei 03, 2012
Luteni Jenerali wa Uganda Andrew Gutti alichukua uongozi wa jeshi la AMISOM siku ya Jumatano (tarehe 2 Mei) wakati wa sherehe za makabidhiano nchini Mogadishu, Umoja wa Afrika ulitangaza katika ujumbe wake.
"Lutenu Jenerali Gutti ataongoza majeshi ya AMISOM katika mapigano yanayoendelea ya kuleta amani na mafanikio kwa watu wa Somalia," balozi wa Umoja wa Afrika (AU) Rodney Kiwa aliwaambia viongozi wa Afrika na Umoja wa Matafia waliohudhuria.
"Pamoja na msaada wa jumuiya ya kimataifa, AMISOM wataendelea kufanya kazi ya kuleta amani na uhuru kwa Somalia kwa ajili ya siku zijazo, ambayo ni muhimu kwa maendeleo katika mapambano ya dunia dhidi ya ugaidi na kutafuta uimara wa kanda," alisema.
Gutti alifanya kazi kwa zaidia ya miaka 26 katika jeshi la Uganda na ataongoza jeshi lililopanuliwa la AMISOM lenye wanajeshi kutoka Kenya, Uganda, Jibuti, Burundi and Sierra Leone. Amepokea kutoka kwa Meja Jenerali Fred Mugisha, ambaye alisimamia ufukuzwaji wa wanamgambo wa al-Shabaab huko Mogadishu.
Jeshi la AMISOM kwa sasa lina wanajeshi 14,400 katika nchi kavu ya Somalia, lakini linaongezeka hadi takriban wanajeshi 18,000.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji