Mei 03, 2012
Waathirika kadhaa wa bomu la kujitoa muhanga la Dhusamareb siku ya Jumanne walipelekwa kwa ndege Ethiopia kwa matibabu, na wengine walipangwa kupelekwa Nairobi, Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti Jumatano (tarehe 2 Mei).
Waathirika walielezwa kuwa na hali mbaya sana baada ya ulipuaji wa bomu la kujitoa muhanga kwenye mgahawa mahali ambapo watunga sheria wenyeji walikutana na raia. Ndege ya kukodi iliwachukua majeruhi kutoka Guri El kuwapeleka kwenda Addis Ababa, Alisema Mkuu wa Wilaya Osman Isse Noor.
Waziri wa Habari wa zamani Ahmed Abdisalan na wabunge Hussein Samatar na Abdirizak Isaac Biihi ni miongoni mwa majeruhi wanaotibiwa huko Ethiopia.
Waathirika wengine watano watapelekwa kwa ndege Nairobi kwa matibabu.
Al-Shabaab walidai kuhusika na shambulio hilo, ambalo liliua watu wanane.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Hii ingepaswa kuwa funzo kwa wafuasi wa taaghuut.