Mabomu ya Al-Shabaab yaua watu 8 Dhusamareb, Mogadishu

Mei 02, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Milipuko miwili ya mabomu yanayodaiwa kutegwa na al-Shabaab yaliua si chini ya watu wanane katika miji ya Dhusamareb na Mogadishu hapo Jumanne (tarehe 1 Mei), liliripoti Shirika la Habari la AFP.

“Yalikuwa mashambulizi dhidi ya adui,” al-Shabaab ilisema katika taarifa yake iliyotuma mtandaoni.

Huko Dhusamareb, wabunge walikuwa wakikutana na wananchi katika mkahawa kujadiliana namna ya kuweka uongozi wa eneo hilo pale mtu mmoja alipoingia na kujilipua mwenyewe. Raia wanne na wabunge wawili waliuawa katika mkasa huo na wabunge wengine wawili ni miongoni mwa waliojeruhiwa.

“Mlipuko ulitokea kwenye hoteli mjini na kuwaua watu kadhaa, wengi zaidi wamejeruhiwa,” alisema kamanda mwandamizi wa wanamgambo Ahlu Sunna wal Jamaa, Mohamed Abudlahi Moalim.

Na huko mjini Mogadishu, watu wawili walikufa baada ya mabomu kulipuka kwenye gari iliyokuwa ikitokea makutano ya barabara ya K4 kuelekea uwanja wa ndege, kwa mujibu wa polisi na mashahidi.

“Hatujui ikiwa watu hao walikuwa wanahusika na mabomu hayo au yalipenyezwa kwenye gari yao bila wao kujua,” alisema afisa wa polisi wa Somalia, Mohamed Said Bare. “Gari haikuharibiwa yote, lakini inaonekana bomu liliwekwa mahali chini ya viti.”

Siku ya Jumatano, Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia iliyalaani mashambulizi ya al-Shabaab dhidi ya raia na wabunge ikiwaita wabunge waliouawa kwenye milipuko hiyo kama “watetezi muhimu wa amani ambao waliwatumikia watu wa Somalia na kuonesha uaminifu wao kwa utumishi wa umma”.

Waziri wa Habari, Posta na Mawasiliano, Abdulkadir Hussein Mohamed, alituma rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha yao na kuwatakia majeruhi siha ya haraka.

“Tuliwashinda al-Qaeda kwenye uwanja wa mapambano na kudhibiti uwezo wao wa kufanya mashambulizi,” alisema. “Hata hivyo, sasa wamejielekeza kwenye mauaji ya mabomu ya kujitoa muhaga ambapo huwalenga raia wasio na hatia.”

Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia imeapa kuendelea na kampeni yake dhidi ya ugaidi nchini kote. Mohamed aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama na “kubakia na hali ya tahadhari na kujikusanya kutunza usalama kwenye maeneo yao”.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • sadk muhammad
    May 3, 2012 @ 05:41:15AM

    Ni wazi kuwa magaidi hao hawatasita wakati wowote karibuni. Ni hakika kwa sababu wao ni magaidi na hawawezi kututumia ujumbe kutuambia kuwa wao hawawezi kushindwa, lakini kweli ni kuwa wako katika hali mbaya na wanataka wabakie katika nchi zetu na wanataka vyombo vya habari viwaelekea wao. Njia pekee ya kuondokana nao ni kuendelea na imani yetu njema kwa Mwenyezi Mungu na kuendelea kufanyakazi kwa bidii katika nchi zetu. Bila shaka wataacha. Enyi vijana, huu ni mchezo wa wema dhidi ya ubaya, nani atachoka mwanzo? Si suala la uchaguzi kwa sisi kuchoka kwa sababu Mungu aepushie mbali, tutaangamia kama taifa. Kwa hivyo ni uchaguzi wao ama kuacha au kusalimu amri kwetu au watakabiliana na majeshi yetu. Mwenyezi Mungu awasaidie watu wema na awaangamize magaidi na tunashukuru kwa mtandao huu mzuri katika kutoa mwangaza juu ya maendeleo ya nchi zetu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo