Kenya yatafuta fedha za ziada kwa ajili ya mahakama

Mei 01, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mahakama ya Kenya imeomba bunge kuidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 16.8 (dola za Kimarekani milioni 202) kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi wa ziada wa mahakama, liliripoti gazeti la Kenya la The Standard hapo Jumatatu (tarehe 30 Aprili).

Fedha hizo zitatumika kuajiri “majaji, mahakimu na makadhi 275 pamoja na wafanyakazi wa sekta ya utaamalu 185 kutuwezesha kutimiza wajibu wetu,” alisema Gladys Shollei, mrajisi mkuu Mahakama Kuu.

Uajri huu wa ziada utairuhusu mahakama kukabiliana na mrundikano wa kesi, alisema. “Huwezi kuendesha mahakama kwa bajeti ya shilingi bilioni 7.9 (sawa na dola za Kimarekani milioni 95),” alisema Shollei.

Ikiwa pendekezo hili litaridhiwa, maafisa wa mahakama watalazimika kufuta mikataba ya wafanyakazi walioajiriwa katika utaratibu wa kukabiliana na mrundikano wa kesi, baadhi yake zikiwa zimeshachukua miaka 20 zikiwa mahakamani.

Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama kupendekeza bajeti ya ziada kwa bunge.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo