Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Polisi wafuatilia ulipuaji wa bomu kanisani Nairobi

Aprili 30, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Polisi nchini Kenya wanamtafuta mtuhumiwa wa kwanza katika shambulio la guruneti katika kanisa la Nairobi siku ya Jumapili (tarehe 29 Aprili), wakilenga juu ya maelezo ya mashuhuda kuwa mtu mwenye umri wa miaka 20 hivi aliondoka kanisani muda mfupi kabla ya mlipuko.

"Polisi wanafuata maelezo muhimu yaliyotolewa na mashuhuda ili kumtambua mshambuliaji,” alisema msemaji wa polisi Eric Kiraithe, kwa mujibu wa gazeti la Kenya la Daily Nation.

Shambulio liliua mtu mmoja katika eneo hilo, na kujeruhi watu 15. Waathiriwa kumi na mbili walipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, ambapo mmoja alikufa kutokana na majeraha wakati wa shambulio, alisema S.M. Monda, daktari mpasuaji katika hospitali hiyo.

“Hili ni tendo la kigaidi,” alisema Makamo wa Raisi Kalonzo Musyoka, aliyekuwa miongoni mwa maafisa wa serikali waliowatembelea waathirika hospitalini. “Inasikitisha kuwa wamefikia hadi ya kushambulia watu hata wakiwa katika ibada. Hata hivyo, tunawaomba watu watulie nchini kote.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • susan
    June 1, 2012 @ 04:43:48PM

    Hili limepitiliza mno lakini Mwenyezi Mungu bado yuko hai na anaona hata pale macho ya binadamu hayawezi kuona, kwa hivyo watenda maovu lazima waelewe kuwa siku yao inakuja wakati ukweli utakapojitokeza wenyewe kama ambavyo chochote kilichomo katika giza kitakuja kwenye mwanga na kila mtu atalishuhudia hilo.

  • Murathi Kah Wendani
    May 1, 2012 @ 04:28:32AM

    Al-Shabaab wameandikiwa kushindwa. Mungu anaziona njia zenu za uovu na hamtafika mbali zaidi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo