Uchunguzi: Malaria ya Afrika yaanza kupinga madawa

Aprili 27, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vimelea vya malaria vinavyoua watu wengi Afrika vimeonyesha kukinzana na madawa mengi yenye nguvu yaliyoko sokoni, watafiti huko London walieleza hapo Ijumaa (tarehe 27 Aprili).

Wanasayansi wamegundua ukinzani huo katika dawa dhidi ya malaria katika uchunguzi wa damu kutoka wagonjwa 11 kati ya 28 ambao waliugua baada ya kutembelea nchi za Afrika chini ya jangwa la Sahara, hayo ni kwa mujibu wa machapisho katika Jarida la Malaria la BioMed Central.

"Ukinzani huo katika majaribio ya maabara kwa kawaida hupelekea kuwepo kwa ukinzani pia katika baadhi ya nyakati kwa mgonjwa," alisema mkuu wa utafiti huo Sanjeev Krishna, kwa mujibu wa AFP. "Hilo linaweza kumaanisha kushindwa katika matibabu, bado tuna haja ya kutathmini zaidi."

Ukinzani huo wa madawa kwa matibabu kumeibua wasiwasi kuhusu madawa kutokuwa na nguvu kwa wagonjwa, hasa katika nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara, ambako aslimia 50 ya vifo vinavyotokana na malaria hutokea kila mwaka.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kulikuwa na vifo 655,000 vya malaria mwaka 2010. Malaria ni ya tano kwa kusababsha vifo vya kawaida katika nchi zinazoendelea.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo