Bodi ya uchunguzi ya Kenya yawafukuza majaji wanne

Aprili 26, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Bodi ya Uchunguzi wa Majaji na Mahakimu ya Kenya imewafukuza majaji wanne waandamizi ambao iliwakuta hawafai kufanya kazi, mwenyekiti wa bodi Sharad Rao alitangaza Jumatano (tarehe 25 Aprili).

Jopo la uchunguzi, lililoundwa mwaka kufuatia vurugu za baada ya uchaguzi, ilipewa kazi ya kuchunguza utendaji haki wa mahakama za Kenya, Redio Capital FM News ya Kenya iliripoti.

Jaji Riaga Omolo, mkuu wa mahakama ya rufaa, alikuwa ni miongoni mwa majaji waliofukuzwa. Omolo alipatikana kuwa na upendeleo katika kazi, pamoja na hukumu zisizolingana katika kesi za kisiasa. “Katika mambo yote ya kisiasa yaliyotangazwa sana, uamuzi wa [Omolo] ulionekana kuwa na upendeleo wa ugandamizaji kuliko kutoa nafasi ya wazi kwa maelezo ya kidemokrasia,”

Majaji wanne waliofukuzwa wana wiki moja ya kukata rufaa ya uamuzi huo. Majaji wengine watano walifutiwa mashitaka na wataendelea na kazi yao.

"Tunaipongeza bodi kwa kazi ambayo wameifanya,” alisema Waziri wa Mambo ya Katiba Eugene Wamalwa. “Hii ni hatua nyingine ambayo tumeichukua kurejesha imani ya wananchi katika taasisi hii muhimu, na kadri tunavyoendelea, kutakuwa na uharibifu wa pande zote, lakini lazima tuhakikishe imani ya wananchi inarejeshwa.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo