Aprili 25, 2012
Halmashauri ya Mji wa Nairobi ilizawadiwa cheti cha Shirika la Kimataifa cha Uthibitisho wa Viwango (ISO) kwa utoaji wa huduma Jumanne (tarehe 24 Aprili), kufuatia jitihada zake za kurekebisha huduma za serikali na kuanzisha malipo kupitia katika njia za elektroni.
"Baraza la Mji wa Nairobi imekuwa kituo cha kwanza cha mji katika Afrika Mashariki na Kati kupata uthibitisho wa ISO,” Karani wa Mji Philip Kisia alisema alipopokea tuzo huko Ukumbi wa Jiji. “Hata hivyo, ushindi huu mkubwa na heshima vinakuja kwa wakati – kila baada ya miezi sita mchakato utakuwa ukipitiwa upya ili kuhakikisha ufuataji, hivyo hakuna nafasi ya kulala.”
Kisia alisema timu yake imeleta mabadiliko katika sekta muhimu tano ikiwa ni pamoja na fedha, teknolojia ya habari na mawasiliano, mipango, uthamini wa mali na rasilimali watu. Pia alitaja mafanikio yake katika kusambaratisha vikundi vya ufisadi.
Kisia alisema mapato ya halmashauri yataongezeka kwa shilingi bilioni 5 (kiasi cha Dola milioni 60) mara mfumo wa malipo kupitia elektroniki utakapozinduliwa wiki chache zijazo, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji