Umoja wa nchi za Ulaya watangaza programu ya ulinzi wa baharini Afrika Mashariki

Aprili 25, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Umoja wa nchi za Ulaya unapanga kuanza programu ili kusaidia kuimarisha ulinzi wa baharini katika Afrika Mashariki jinsi mashambulizi ya maharamia yanavyopungua katika kanda, Balozi wa EU Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi, alitangaza siku ya Jumanne (tarehe 24 Aprili).

Programu ya kanda ya kujenga Uwezo wa Baharini, ambayo inahusisha Somalia, Kenya, Tanzania na Djibouti, Ushelisheli na Mauritius, itaendeshwa kwa mwaka mmoja hadi miwili, kwa uwezekano wa kuongezwa, Sebregondi alisema, kwa mujibu wa Bloomberg. Huko Somalia, itasisitiza mafunzo ya polisi na mahakama ili kuwezesha nchi kushughulikia makosa ya uharamia ndani ya nchi.

Mashambulizi ya kiharamia katika pwani ya Somalia yamepungua kutoka matukio 97 hadi 43 katika robo ya kwanza ya 2012, kwa mujibu wa Ofisi ya Mambo ya Bahari ya Kimataifa.

EU pia inapanga kutumia euro milioni 16 (Dola milioni 21) miaka miwili ijayo katika programu yake ya kupambana na uharamia katika pwani ya Somalia ili kulinda meli za chakula cha msaada za Umoja wa Mataifa zinazoingia nchini.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo