Vikosi vya ulinzi vya Somalia vyaua wafuasi wanne wa al-Shabaab

Aprili 25, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya ulinzi vya serikali ya Somalia vimewapiga risasi na kuwaua wafuasi wane wa al-Shabaab huko Mogadishu Jumanne (tarehe 24 Aprili) baada ya wapiganaji kuwaua raia wawili katika sehemu mbalimbali ya mji, Jeshi la Ulinzi la Taifa la Somalia limesema katika taarifa yake.

Vikosi vya ulinzi viliwaua wapiganaji wawili, ambao walikuwa na bastola, baada ya kumuua mtu aliyekuwa anatoka msikitini katika kijiji cha Blacksea. Saa chache baadaye, vikosi vya ulinzi viliwapiga risasi na kuwaua wapiganaji wengine wawili katika kijiji cha KPP baada ya kumuua kijana. Vijiji vyote viko katika wilaya ya Hodan.

Wapiganaji walipewa nafasi ya kujisalimisha kwa vikosi vya ulinzi, lakini walikataa, kwa mujibu wa Jeshi la Ulinzi la Taifa la Somalia.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo