Aprili 24, 2012
Kituo cha Doha cha Uhuru wa Vyombo vya Habari kilitoa dola 9000 kwa msaada wa matibabu kwa waandishi wa habari sita waliojeruhiwa hapo tarehe 4 Aprili kwa bomu la kujitoa muhanga katika Jengo la Maonyesho la Taifa la Mogadishu, Redio RBC ya Somalia iliripoti hapo Jumatatu (tarehe 23 Aprili).
Chama cha Taifa cha Waandishi wa Habari wa Somalia (NUSOJ) iligawanya pesa hizo Ijumaa iliyopita kwa Said Warsame (Shuuriyaako), Deeqo Mohamed Ahmed, Ahmed Ali Kahiye, Hamdi Muhumad Hassan, Ayaan Abdulle Guure na Makamo wa Raisi wa NUSOJ Saleiban Sheik Ismail.
Warsame, aliyeungua vibaya mwili mwake, alipewa dola 2000 ili zimsaidie kutibiwa nje ya Somalia.
Katibu Mkuu wa NUSOJ Mohamed Ibrahim alikabidhi pesa hizo kwa mkurugenzi wa Royal International Television Abdulkadir Dulyar, ambaye aliziwasilisha katika familia ya Warsame.
"Kama unavyooana… wenzetu hawawezi kutibiwa Somalia na kwa niaba ya vyombo vya habari, ninayaomba mashirika yote na asasi za serikali zilizoguswa na suala hili kuwasaidia waandishi wa habari wa Somalia waliojeruhiwa,” Dulyar alisema.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji