Aprili 22, 2012
Mahakama Kuu ya Kenya ilitoa uamuzi siku ya Ijumaa (tarehe 20 Aprili) kwamba tafsiri ya "ughushi" katika Sheria ya Kuzuia Ughushi ni pana mno na itaweza kuzuia upatikanaji wa dawa za kijenasi.
"Sheria haiko wazi na inaweza kupunguza upatikanaji wa dawa za kijenasi za bei nafuu, kwakuwa sheria imeshindwa kutofautisha kati ya ughushi na dawa za kijenasi," Jaji Mumbi Ngugi alisema wakati wa kutoa hukumu.
Mahakama Kuu ililiomba Bunge kupitia sheria ili kulinda dhidi ya utaifishaji wa dawa za kijenasi kwa kisingizio cha kukabiliana na dawa za kughushi. Hukumu pia ilieleza kwamba haki za kumiliki utaalamu hazipaswi kuzidi haki za kuishi na afya.
Mwishoni mwa mwaka jana, takriban watu milioni 1.6 nchini Kenya walikuwa wakiishi na VVU, kutokana na taarifa za shirika la UNAIDS, Programu ya Pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu VVU/UKIMWI. Wakenya takriban 743,000 wanastahili kupata matibabu ya kupunguza makali, wakati 539,000 wanayapata.
"Watu wengi nchini Kenya wanazingatia dawa zenye ubora za kijenasi kwaajili ya maisha yao ya kila siku," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibé. "Uamuzi huu umeweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba dawa za kuokoa maisha zinapatikana."
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji