Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Kufanikiwa kwa mashambulizi ya kiharamia katika Bahari ya Hindi kwapunguzwa

Aprili 22, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kulikuwa na mashambulizi machache ya kiharamia yaliyofanikiwa katika Bahari ya Hindi katika robo ya kwanza ya mwaka 2012 kuliko katika kipindi kama hicho mwaka jana, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Vikosi vya Maji vya Umoja wa nchi za Ulaya huko Somalia (EU NAVFOR).

Ripoti ilitaja mashambulizi 27 ya kiharamia kati ya Januari na Aprili, yakilinganishwa na 91 mwaka jana. Kiwango cha kufanikiwa kwa uharamia kilishuka hadi asilimia 14 katika robo ya kwanza mwaka jana, kikilinganishwa na asilimia 27 katika kipindi kama hicho mwaka 2010 na asilimia 28 mwaka 2009.

Kushuka kwa shughuli za uharamia ni kutokana na ongezeko la ulinzi wenye silaha katika meli za biashara, kuwepo kwa vikosi vya majini vya kigeni katika njia za meli na mashirika ya meli kuongeza umakini katika taratibu nzuri za usimamizi, kwa mujibu wa ofisa habari wa EU NAVFOR Timo M. Lange.

Ili kuzuia uharamia na uvamizi wa kutumia silaha, EU NAVFOR imetoa wasindikizaji kwa meli 150 za Programu ya Chakula Duniani na meli 126 za AMISOM. Lakini bado maharamia wanashikilia meli tisa na mateka 242.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo