Madaktari Wasio na Mipaka wasimamisha miradi mipya nchini Somalia

Aprili 17, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kikundi cha kimataifa cha misaada ya kibinadamu, Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), hawataanza miradi mingine yoyote mipya isiyo ya dharura nchini Somalia mpaka wafanyakazi wawili wanaoshikiliwa mateka waachiwe, redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti Jumatatu (tarehe 16 Aprili), ikinukuu taarifa ya kikundi hicho.

Blanca Thiebaut na Monserrat Serra wanashikiliwa mateka nchini Somalia toka mwezi Oktoba 2011, wakati walipotekwa kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab katika jimbo la Kaskazini Mashariki nchini Kenya, ambalo linawahifadhi wakimbizi wa Somalia zaidi ya 450,000.

MSF kwa sasa wanaendesha miradi ya tiba nchini Somalia katika vituo 22 kati kusini mwa Somalia. Taarifa hiyo ilisema kuwa shirika hilo litaendelea kujishughulisha na dharura za kuokoa maisha.

Thiebaut na Serra waliripotiwa kuonekana mara ya mwisho Lower Shabelle mwezi Disemba.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo