Aprili 13, 2012
Al-Shabaab, kikundi washirika wa al-Qaeda, kilimuua mpiganaji jihadi aliyezaliwa Marekani Omar Hammami hapo tarehe 5 Aprili, kwa mujibu wa ripoti zisivyothibitishwa bado za vyombo vya habari.
Hammami, aliyejulikana kama Abu Mansour al-Amriki, alisema anahofia maisha yake kutoka kwa viongozi wengine wa al-Shabaab kwa sababu ya tofauti za kimkakati na kiitikadi katika tarifa iliyotolewa mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa mtandao wa Somalia wa Gedo Online, Hammami aliyekuwa pekee kutokuwepo katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi wakuu wa al-Shabaab huko Baraawe.
Inasekena al-Shabaab walikuwa wakimuwinda Hammami baada ya kuondoka kwake Marka katika eneo la Lower Shebelle. Inasemekana alikatwa kichwa hapo hapo na kuzikwa katika eneo moja baina ya Marka na Baraawe.
Kwa mujibu wa ripoti hizo, mauaji hayo yanayotajwa yaliwakasirikisha baadhi ya viongozi wa al-Shabaab, ambao walimshutumu kiongozi wa al-Qaeda Ahmed Abdi Godane kwa kuamrisha mauaji hayo.
Kikundi cha wapiganaji wa kigeni na wananchama wengine wa juu wa al-Shabaab, akiwemo Fuad Mohamed Khalaf, anayejulikana pia kwa jina la Fuad Shongoole, wanasemekana kukimbilia katika milima ya Galgala kufuatia habari za mauaji hayo.
Viongozi wengine walioondoka baada ya kusikia habari hizo ni pamoja na Hassan Dahir Aweys na Mukhtar Robow, mtandao wa Gedo Online uliripoti.
Aweys karibuni aliwashutumu viongozi wengine wa al-Shabaab, akiwemo Godane, kwa kumwaga damu ya Waislamu na kuua wananchi wasio na hatia kwa jina la Uislamu. Alivitaja vitendo vya viongozi wa al-Shabaab kuwa vinajitoa katika Uislamu.
Wachambuzi wa Somalia wanasema kuwa kikundi cha al-Shabaab washirika wa al-Qaeda kiko ukingoni mwa kuvunjika kutokana na migawanyiko mikubwa ya ndani iliyosababishwa na vipingamizi vya hivi karibuni ya kijeshi.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ninawahurumia, wamesukumwa na mgawanyiko wao MKUBWA (ubaguzi wa kikoo, chuki na mengineyo). Watu wenye msimamo na itikadi kali wameyatumia hayo na hawataacha mauaji, kwa sababu hawana nia ya kufanya hivyo; kama wangekuwa wanataka kuacha mauaji wangekwisha fanya hivyo miaka mingi iliyopita. Hata marehemu SIAD BARRE aliwaacha na kuwalaani na kama hawakusali na kuomba laana hiyo ifutike, hakuna mauaji yatakayosimama.
Ninamuonea hutuma masikini huyu ambaye mwanzo alipotosha lakini baadaye akauliwa. Ninashangaa kwa nini hakuweza kuwatoroka? Pengine ilikuwa wakati wake wa kufa umefika na asingeweza kuishi zaidi ya hapo. KWAHERI
mimi ningepena hawa watu wenye siyasa kali hatusemi ni waislamu wenye dini kali uslamu hauna ukali siasa na dini ni tafauti kabisaa naomba wislamu msichanganye dini na siasa au msiabukizwe huko ni marathi makubwa waislamu ni wamoja inshalaa hakuna kupinga hiyo mimi niko hargaisa nasikitika nikisikya kuna somali land na butland pia hawa watu wanayo jilipuwa watakweda wapi huko watajuta sana nawasitikiya sana
Al-Shabaab mwanzoni walikuwa wanapigana kwa sababu zinazohusiana na siasa na utawala lakini sio kwa sababu za kidini kama wanavyodai. Abu-Mansour alifikiria kuwa walikuwa wanapigana kweli kwa ajili ya dini lakini baadaye akagundua kuwa walikuwa wanahamasihswa na siasa. Ukweli ni kuwa kikundi hiki kinasambaratika kwa kasi sana na ningependa kinasambaratika zaidi ya hivyo, kwa uwezo wa Mungu. Amen.
Pengine alifikiria kulikuwa na vita vitakatifu vya kweli nchini Somalia wakati alipokuja. Alipoona kile wanachofanya alijaribu kuwazuia lakini hakujua kuwa hakuna mtu wa kuweza kikuzuia kikundi hiki kipotofu. Ninamsikitikia masikini huyu aliyefikiria kuwa al-Shabaab imeundwa na Waislamu wa kweli. Hakujua kuwa ni mapagani ambao hawaheshimu dini yoyote. Naomba kwa Mwenyezi Mungu.
Ni ushahidi gani uliopo wa kuthibitishwa kuwa uvumi huu ni kweli hasa? Ukweli utabaki kuwa mashetani hawa hawawezi kutabirika. Pengine ni mpango tu lakini kwa njia yoyote ikiwa amekufa, kwa hivyo hongera kwa wale waliofanya hivyo kwani na wao watapitia moto huo huo....hakuna kitu kama vita vitakatifu. Mnyama muovu yule!!!!!
Ni maumbile kuwa kitu kikishafika juu huanguka, kikundi cha washirika wa al-Qaida, al-Shabaab baada ya miaka kadhaa katika uongozi sasa wameanza kutawanyika kutokana na mzozo wa kimaslahi na kupigania uongozi. Watu kama Hammami wamefanya maovu katika ardhi ya Somalia na sasa wanapata adhabu wanayostahiki kutoka ndani ya kikundi chenyewe, lakini naamini kuwa huku ni kukamatwa na Mwenyezi kusikowahi kutokea kwa watu hawa wapuuzi kwa sababu haki ya Mungu ni kuwawinda watu waovu kama hawa. Tutafurahi sana kusikia habari nzuri kama hizi na tunasubiri kusikia habari nyingine nzuri mwezi huu unaokuja.
Mnatania hadi mwisho wa dunia lakini mtalia milele katika moto wa jahanam.
Mwongo, hamko sahihi kabisa, mnasema nini? watu wanafki (munaafiq)siku zote mnasema kama hivyo hivyo.
Huyu mtu alikuwa mujahidina na kazi yake ilikuwa kuua watu. Ni faida yetu kuwa ameuliwa na pia ni faida yetu wakati kikundi kilichokosa radhi kinapogawanyika kutokana na uchoyo wao. Uislamu ni dini kama zilivyo dini nyingine lakini inachafuliwa na wale wanaojiita mujahidina ambao wametiwa kasumba na wakubwa wao ambao kwa kweli wao hawako tayari kufa kwa sabau yoyte ile na ndio maana ilichukua miaka kumuua Osama.
Mwenyezi Mungu ni Mkubwa! Magaidi wanauana wao kwa wao! Hongera kwa Wasomalia na waislamu kwa jumla kwa sababu mshenzi ameuliwa na tumeondokana naye milele kwa sababu alikuwa sehemu ya al-Shabaab. Ingia motoni wewe na wafuasi wako na muishi milele motoni mpaka Siku ya Hukumu. Mmelaaniwa katika dunia hii na akhera kwa kila mlichofanya kwa watu wasio hatia na ambao hawakufanya uhalifu au kosa lolote. Hii ndio hatma kwa kila anayefanyakazi ya ugaidi. Ninawashauri wote wanaofanyakazi nao wajisalimishe na wajikabidhi wenyewe kabla hawajachelewa sana.
Abu-Mansur ni Muislamu na sitofanya dhambi kwa kusema jambo baya dhidi yake. Sitomnyanyasa wala kumsifu bali Mungu amuadhibu kwa matendo yake. Inawezekana kuwa al-Shabaab wamemuua mtu mweuepe na sishangai kwa nini kwa sababu wameshaua watu wengi bora zaidi kuliko yeye miongoni mwa Wasomali na daima sitamsahau mtu mkubwa kama vile Sheikh Mohammad Abdirahman, aliyeuliwa huko Bosasa mwaka jana wakati akiwa njiani kutoka msikitini baada ya suala ya alfajiri, mawaziri waliowauwa katika mlipuko wa Hoteli Shamow. Wanachama wa al-Shabaab si Wasomali na hawawapendi Wasomali. Kama ni Wasomali kwa nini wauwe Wasomalia? Watawatawala nani ikiwa wanaendelea kupiga mabomu ya kujitoa muhanga na kuua watu kwa halaiki? Watatawala miti, ardhi tupu na sehemu zisizo kitu kwa sababu ikiwa wanaendelea kuua watu namna hii, hakuna atakayebakia nchini Somalia muda mfupi ujao. Ninamuomba Mungu afanye atulinde kutokana na majanga haya na atulinde na matendo maovu yanayofanywa na al-Shabaab. Mimi ni ndugu ninayeishi Hargeisa, Somaliland na ambaye ninawapenda ndugu zangu wanaoishi kusini ya Somalia ambao wanavumilia matatizo kwa muda mrefu.
Ninaunga mkono wazo hili kuhusu mgawano sawa wa mali.
Hilo lilitarajiwa kutokea, kama ambavyo wezi wowote wanaoiba na kuua, baadaye wanakwenda kupigana dhidi ya wao kwa wao juu ya kile walichoiba. Mungu waunganishe na Osama Bin Laden, Zarqawi, na yeyote anayewafuatia! Tunamuomba Mungu kuwaokoa Wasomalia na Waislamu kwa jumla kutokana na maovu ya al-Qaeda, “Al-Shabaab” na kikundi chochote cha kigaidi!
Habari nzuri...Mwenyezi Mungu awafanye wauwane wao kwa wao ili Waislamu waondokane nao. Ni watu wapumbavu tu wanaostahiki kuuliwa na kuchomwa moto.
Kile ambacho kimejengwa kwa uongo hubakia kuwa uongo! Kile kilichojengwa kwa chuki huisha! Kikundi cha “Al-Shabaab” kimejaa chuki na ni jambo la maumbile kuwa kinavunjika, wataishia kupigana wao kwa wao, kwa sababu mawazo yao yamejengeka katika kuwaweka kando wengine, na kuwafanya sio muhimu. Ni jambo la kimaumbile kuwa pale wanapowafanya wengine waende uhamishoni, watu katika kikundi chao watahama vilevile, mmoja baada ya mwingine. Hii ni kwa bahati yetu nzuri na kwa msaada wa Mungu. Kuran Takatifu inasema, “Kwa jina la Mungu mwingi wa Rehema, mwenye Kurehemu, wanadanganya na kufanya hila, lakini Mungu ni mbora zaidi wa hila.” Mwenyezi Mungu ndiye mkweli.
Amani iwe juu yenu. Wale wote wanaokubaliana na kuwadhuru watu kwa sababu hii mwisho watachomwa moto. Aina ya vita vilivyokuwa vinafanywa na al-Ameriki nchini Somalia si vya haki na havikuwa vita juu ya dini ya Kiislamu. Sioni kuuliwa kwake kuwa ni jambo baya kwa sababu na yeye pia alikuja Somalia kuua wengine ambao hawakumkosea lolote. Ikiwa ni kweli ameuliwa, kwa hivyo, anasyahiki. Mzee mtu mzima, Hassan Dahir Aweys amezingirwa na hana pa kukimbilia kutafuta hifadhi. Hakuna hata wakati mmoja ambao tumemsikia Hassan ahir akisema, kuua Waislamu KUMEKATAZWA. Alikuwa anaishi Mogadishi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza nchini Somalia lakini daima hakuzungumzia juu ya mauaji ya Wasomali wenzake hasa na kikundi cha ukoo wake Mogadishu na zile nyombo nzuri alizoanza kuziimba peke yake siku hizi haziwezi kumfanya aonekane hana makosa ya ukikukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya jamii ya Somalia. Ikiwa hii ni kweli kuwa mwana wa Shongole alikimbia kutoka mafichoni, hapo, ningependa kumpelekea ujumbe kuwa hatutamuacha katka Milima ya Galgala na tutmuua mara tu baada ya kumkamata akiwa hai kwa sabau tuliambiwa wapi alikimbilia, ni tofauti na kusini na maeneo ya kusini ya Somalia, yanayokaliwa na watu waoga ambao laikuwa anawatisha. Lazima ajuwe kuwa watu wa Puntland ni tofauti na watu wanaoishi eneo la kusini ya Somalia. Mwana wa Shongole asili yake ni Puntland lakini hilo halitamsaidia leo kwa sababu uhalifu aliotenda dhidi ya watu wa Somalia ni mkubwa kuliko asili yake na pia hatahifadhiwa. Nmesikia Wasomali wengi wakisema kuwa Godane anafanyakazi kwa ajili ya wageni walioko nje ili kuzua mzozo nchini Somalia na ninaweza kuamini kuwa habari hii ni kweli kwa sababu ya matendo yasiyo huruma anayofanya.