Aprili 10, 2012
Mamlaka ya Viwanja vya ndege ya Kenya (KAA) ilitangaza siku ya Jumatatu (tarehe 9 Aprili) kwamba imewafukuza wafanyakazi waliokaidi kurejea kazini kufuatia mgomo mwishoni mwa wiki, Redio Capital FM ya Kenya iliripoti.
"Wafanyakazi wote ambao bado wanajihusisha na mgomo usio halali wamechukuliwa kwamba hawajafika kazini na kwa kifupi wamefukuzwa," KAA ilieleza katika waraka wake.
KAA imesema kwamba zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wake 1,500 walioungana wamerejea kazini kufuatia mgomo mfupi ambao ulianza Ijumaa.
"Tunachukua fursa hii kuuhakikishia umma kwamba huduma katika viwanja vyetu vyote vya ndege zimeendelea bila vikwazo vyovyote," ulieleza waraka huo. Uongozi na wakala wa serikali walichukua hatua za dharula wakati wa mgomo, waraka ulieleza.
Nicholas Baraza, katibu wa Umoja wa Wafanyakazi wa Viwanja vya ndege na wafanyakazi mwega, alisema mgomo bado unaendelea. "Hadi labda tutakapokubaliana na KKA kuhusu mapato kwa kanuni ya kazi, hakuna jinsi ambayo wanachama wetu watarejea kazini," alisema.
Chama kilisema siku ya Jumatatu kwamba kitaendelea na wito wake kwa nyongeza ya malipo ya asilimia 25 kwa wafanyakazi.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji