Aprili 10, 2012
Serikali ya Somalia inaendelea kuikomboa nchi dhidi ya ugaidi na inaelekeza vita dhidi ya al-Shabaab katika “ngome zao nchini humo”, ilitangaza Serikali ya Mpito ya Shirikisho la Somalia hapo Jumatatu (tarehe 9 Aprili).
Katika taarifa rasmi, serikali hiyo imetaja mifano ya wilaya zilizokombolewa hivi karibuni za Bay, Bakol, Hiiraan na Galgadud kama sehemu za mkakati “kuuharibu uwezo wa al-Shabaab/al-Qaeda na kupunguza kitisho chake”.
Serikali ilitangaza kwamba inaelekea kwenye mkoa wa Bay, ikichukuwa hivi karibuni udhibiti wa Qansax-dheere, Burhakaba na Ufuroow.
Ili kudumisha amani na utulivu katika wilaya mpya zilizotekwa, vikosi vya serikali na vya Umoja wa Afrika wameweka vikosi vyao katika miji mikubwa na midogo “kutanua nguvu za serikali nje ya mji mkuu na kumaliza ugaidi wa al-Qaeda.”
Katika habari nyingine, maafisa wa kijeshi kutoka Sierra Leone waliomo kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika waliwasili katika mkoa wa Gedo hapo Jumatatu, iliripoti Redio Mogadishu. Wanajeshi wa Sierra Leone wanatarajiwa kujiunga na AMISOM baada ya nwezi wa Juni.
Maofisa hao waliyatembelea maeneo ya vikosi vya usalama vya Somalia yaliyotawaliwa kutoka al-Shabaab hivi karibuni na kukutana na wawakilishi wa Serikali ya Somali Garbaharey kujadiliana mkakati wa kuwashinda al-Shabaab katika mkoa huo, alisema mbunge Mohamed Sayid Adam.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji