Idadi ya vifo kutokana na shambulio la jumba la maonesho Mogadishu yaongezeka hadi sita

Aprili 09, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Waathirika wawili zaidi kutokana na shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika Jumba la Maonesho la Taifa mjini Mogadishu siku ya Jumatano walikufa mwishoni mwa wiki kutokana na majeraha, wakiongeza idadi ya vifo kuwa sita, Mtandao wa Habari wa Garowe Online ya Somalia imeripoti Jumapili (tarehe 8 Aprili).

Mbunge Mowlid Ma'aney Mohamud na Faisal Haji Elmi, mshauri wa Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali, walifariki katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, ambako walihamishiwa kwa ajili ya matibabu baada ya kukaa katika Hospitali ya Medina ya Somalia.

Siku ya Jumapili, Ali alitoa taarifa ya rambirambi kwa familia za waathirika akiuita uvamizi kuwa ni mbaya, shirika la habari liliripoti. “Faisal alijitolea katika kuimarisha na kuendeleza serikali hii na Mungu atampeleka peponi,” taarifa hiyo ilisema.

Hali kadhalika, wabunge wametoa rambirambi zao kwa familia ya mwenzao aliyefariki, Mohamud, wakisema wamempoteza shujaa, Redio RBC ya Somalia iliripoti.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo