Aprili 06, 2012
Wanajeshi wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika (AMISOM) kimepeleka katika mji wa Baidoa hapo Alhamis (tarehe Aprili 5) ikiwa ni mara ya kwanza kwa kikosi hicho kufanya kazi nje ya mji wa Mogadishu tangu kilipowasili nchini Somalia miaka mitano iliyopita.
Wanajeshi 100 kutoka Burundi na Uganda walipelekwa katika mji huo ambao ulitekwa na wanajeshi wa Ethipoia na Somalia kutoka mikononi mwa wapiganaji wa al-Shabaab wenye uhusiano na al-Qaeda hapo mwezi Februari.
"Wanajeshi hawa 100 ni mwanzo wa timu ya wanajeshi 2,500 wa AMISOM ambao watapelekwa huko kwa awamu. Timu ya hivi sasa itapiga kambi pamoja na wanajeshi wa Ethiopia walioko Baidoa,” alisema msemaji wa AMISOM, Paddy Ankunda, katika taarifa yake.
"Leo tumepiga hatua moja kubwa mbele kwa ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia na kwa kila anayetaka amani nchini humu,” alisema naibu kamanda wa kikosi cha AMISOM, Audace Nduwumunsi. Alisema vikosi vya Umoja wa Afrika vitachukuwa nafasi ya vikosi vya Ethiopia katika maeneo yaliyotwaliwa kutoka mikononi mwa al-Shabaab.
Al-Shabaab inakabiliwa na mashambulizi ya vikosi vya eneo hilo, ambapo wanajeshi wa Kenya wanawashambulia kutoka kusini huku wale wa Ethiopia wakiwashambulia kutokea kusini na magharibi ya Somalia. Katika miezi ya hivi karibuni, wanajeshi wa Ethiopia walisaidia kuzikomboa ngome nne za al-Shabaab.
Nduwumunsi alikuita kutanuliwa kwa upelekwaji wa vikosi vya Umoja wa Afrika kama “ncha kali ya mshale ambayo itaingia ndani ya moyo wa maeneo yanayothibitiwa sasa na wapiganaji wa al-Shabaab wanaoungwa mkono na al-Qaeda…. Wanapoteza nguvu na wanapoteza marafiki Somalia nzima.”
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji