Aprili 05, 2012
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, hapo Jumatano (Aprili 4) aliitaka serikali kuweka sheria ndogo ndogo za kusaidia kuwainua wafanyabiashara wadogo wadogo, liliripoti gazeti la nchi hiyo la Daily Nation.
Taasisi za umma lazima zishirikiane kuinua maisha ya wananachi, alisema Rais Kibaki katika uzinduzi wa soko jipya la Kamukunji huko Nyeri. Soko hilo lililojengwa na serikali kwa gharama ya shilingi milioni 223 (dola milioni 2.6 za Kimarekani), lina maduka 500 kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, mkahawa na sehemu ya huduma.
Soko hilo lilijengwa kufuatia ushirikiano wa Wizara ya Nyumba, Mpango wa Kupandisha Daraja Maeneo ya Mabanda na Baraza la Manispaa la Nyeri.
Kibaki alisema soko hilo jipya litakuwa kama kiunganisho baina ya uzalishaji wa soko na uinuaji wa uchumi wa Nyeri. Soko hilo litawaondoa wafanyabiashara wanaorandisha bidhaa zao mitaani na kuwaweka pamoja na hivyo kutoa mazingira ya kufanya kazi pamoja, alisema Rais Kibaki.
Kibaki aliyataka mashirika ya serikali kuiga ushirikiano kama huu ili kuinua utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Alisema mageuzi kama hayo yanahakikisha kuwa maeneo ya vijijini yanapata ukuwaji wa uchumi na hivyo kuwavutia wawekezaji, na matokeo yake kuibadilisha sekta ya kilimo ya Kenya kutoka ile inayotegemea mazao ya chakula kwenda ile inayotilia mkazo biashara.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji