Waziri mkuu wa Somalia: Somalia haitatishwa na al-Shabaab

Aprili 05, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali alisema shambulizi katika Jumba la Maonesho la Taifa hapo Jumatano (tarehe 4 Aprili) hakutorejesha nyuma juhudi za serikali za kupambana na al-Shabaab, gazeti la mtandaoni la Somalia la Garowe Online liliripoti.

"Hii haitapunguza wala kuturejesha nyuma kutoka njia yetu," Ali alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mogadishu saa chache baada ya mlipuko. Al-Shabaab wanakabiliwa na kushindwa, na ndio maana wanajikaza katika kudhoofisha na kutumia mbinu chafu kama hizi."

Kiasi cha watu sita waliuwawa na 10 kujeruhiwa wakati mwanamke mwenye umri mdogo aliporipotiwa kujitoa muhanga kwa kuvaa mkanda wenye mabomu, ambaye alimleng Ali na Viongozi wengine wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa kituo cha televisheni ya Taifa.

"Wananchi wasio na hatia waliuawa katika mlipuko huo na serikali ya TFG inashughulikia kuboresha usalama wetu ili mashambulio kama haya yasitokee ten," alisema Ali, huku akiwashukuru viongozi wa usalama, wanajeshi na mapolisi kwa kufanikisha uzuiaji wa mashambulio mengine kama hili huko Mogadishu mara kadhaa.

Majeshi ya Usalama yapo katika hadhari ya hali ya juu jijini, kaimu mkuu wa usalama wa Mkoa wa Banaadir, Warsame Mohammed Jodah, aliiambia Shabelle ya Somalia siku ya Jumatano.

Mogadishu imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya mauaji na makombora tangia al-Qaeda-iwashirikishe katika matukio ya al-Shabaab yaliyotelekezwa katika makambi ya kudumu ya al-Shabaab katika mji mwezi Agosti na kurejea kwa mbinu za mapigano ya msituni.

Waziri mkuu alituma salamu zake za rambirambi kwa familia za wale waliouawa katika mlipuko ikiwa ni pamoja na rais wa Kamati ya Olimpiki ya Somalia Adaan Haaji Yabaroow "Wiish" na kiongozi mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Somalia Said Mohamed Nur "Mugaanbe".

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo