Uwanja wa michezo wa Kisumu kuboreshwa

Aprili 03, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Uwanja wa Michezo wa Moi huko Kisumu Kenya utaboreshwa kwa kutumia shilingi milioni 42 (Dola za Kimarekani 500,000) kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Jumatatu (tarehe 2 Aprili).

Fedha zitalipwa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) kama sehemu ya jitihada za Lengo la Mradi lililokusudiwa kuchangia programu za maendeleo ya mpira wa miguu kwa nchi zinazoshiriki.

FKF litatumia fedha hizo kuufanya uwanja huo kuwa wa kisasa, kujenga ukuta wa mzunguko na kukarabati vyumba vyenye makabati ya kuhifadhia vitu na maboresho mengine. Baada ya ukarabati huo, Uwanja wa Michezo wa Moi utakuwa wa tatu nchini Kenya kufikia viwango vya mahitaji ya FIFA kwa ajili ya mashindano ya michezo ya kimataifa.

"Kama shirikisho, tumefurahishwa mno na FIFA kukubali kukisaidia fedha chama chetu," alisema mwenyekiti wa FKF Sam Nyamweya.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • BARASA SAUL
    April 4, 2012 @ 04:38:04AM

    Angalau Kenya imeanza kupiga hatua miongoni mwa nchi za dunia ya tatu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo