Al-Shabaab washambulia msafara wa magari yenye chakula ya Shirika la Msalaba Mwekundu huko Gedo

Aprili 03, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Al-Shabaab Jumanne asubuhi (tarehe 3 Aprili) walishambulia kwa kuvizia malori kutoka Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) ambayo yalikuwa yamebeba msaada wa chakula kwa mkoa wa Gedo, Serikali ya Mpito ya Sirikisho ya Somalia (TGF) ilisema.

Msemaji wa jeshi la TFG Aden Ahmed Hirse alisema msafara huo wa malori yaliyokodiwa na ICRC yalishambuliwa katika barabara inayounganisha wilaya za Elwak na El-Adde, kwa mujibu wa Mtandao wa Habari wa Shabelle wa Somalia.

Hirse alisema dereva wa Kisomali aliuawa katika shambulio hilo. Vikosi vya TFG vilifika katika eneo la tukio na kufanya operesheni ya ukaguzi kuwasaka washambuliaji, alisema.

Ofisa wa ICRC alisema msaada wa kibinadamu wa chakula ulikusudiwa kwa familia za Kisomali zilizoathirika na ukame huko magharibi kusini mwa Somalia.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo