Ushoroba wa Afgoye wafunguliwa upya baada ya mapigano huko Daynile

Aprili 01, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Somalia imeiondoa moja ya ngome za al-Shabaab iliyobakia karibu na Mogadishu Jumamosi (tarehe 31 Machi), baada ya mapigano ya siku moja kati ya wapiganaji na wanajeshi wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) wakisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika, wakazi wenyeji waliiambia AFP.

Familia za Somalia walitumia nafasi ya utulivu katika mapigano kuondoka katika wilaya ya Daynile nje ya Mogadishu, ambako mapigano ya Ijumaa yaliua takribani watu kumi, kwa mujibu wa Mtandao wa Habari wa Shabelle wa Somalia. Daynile inasaidia kufika katika ushoroba wa Afgoye, barabara inayounganisha Mogadishu na mkoa wa Lower Shabelle.

Katika wiki chache zilizopita, maelfu ya wakazi wameondolewa Daynile kabla ya shambulio liliotarajiwa kufanywa na vikosi vya AMISOM na Somalia.

Kamanda wa jeshi la TFG Abdullahi Yare, ambaye yuko katika kituo cha ukaguzi cha Afgoye, alisema shughuli zimerejea katika hali ya kawaida katika njia ya Afgoye baada ya kuwa imefungwa kutokana na mapigano, Shabelle iliripoti. Wakazi waliithibitishia AFP kwamba barabara ilifunguliwa tena.

Misheni ya Umoja wa Afrika huko Somalia ilisema siku ya Ijumaa kwamba vikosi vya muungano vimeiteka wilaya kutoka kwa al-Shabaab.

"Operesheni ya kijeshi huko Daynile ilikuwa ya mafanikio na mabaki ya washirika wa al-Qaeda waliondolewa,” kamanda wa jeshi la TFG Abdikarim Yusuf Dhego-Badan aliwaambia waandishi wa habari. “Vikosi vyetu sasa viko karibu katika kila sehemu ya wilaya na hali ni ya utulivu.”

Al-Shabaab nao pia walidai kushinda katika mapambano.

Kikundi cha msaada wa matibabu cha Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) kilisema hospitali ya Daynile ilishambuliwa siku ya Ijumaa, na kutoa wito kwa pande zinazopigana kuheshimu hali ya hospitali kutokuwa upande wowote katika vita.

"Wodi ya dharura na sehemu moja ya chumba cha upasuaji katika hospitali hiyo, ambako MSF wamekuwa wakifanya kazi tangu 2006, vilishambuliwa na kusababisha uharibifu mkubwa,” kundi hilo lilisema katika kauli yake.

Hakuna madaktari au wagonjwa waliojeruhiwa. Wagonjwa wote 19 na wafanyakazi 48 kwa sasa wamejificha ndani ya wodi wakijikinga na mapigano, MSF walisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo