Aprili 01, 2012
Si chini ya mtu mmoja aliuawa na 18 kujeruhiwa katika mashambulio mawili yaliyolenga mkusanyiko katika kanisa huko Mtwapa na katika mgahawa huko Mombasa Jumamosi (tarehe 31 Machi), kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na maofisa wa jeshi la polisi.
Polisi walisema kifaa cha mlipuko, kinachowezekana kuwa ni kombora, kilirushwa katika mkusanyiko huko Mtwapa muda wa kama saa 2 usiku. “Watu kumi na sita walijeruhiwa, wawili walijeruhiwa vibaya, na mmoja alikufa,” Nelly Muluka, msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu aliimbia AFP, akiongezea kuwa majeruhi wamebakia hospitalini.
Mkuu wa polisi wa jimbo la Pwani Aggrey Adoli aliiambia AFP kuwa kombora la pili lilirushwa kwenye mgahawa huko Mombasa” dakika chache baadaye, lilijeruhi watu watatu, akiwemo ofisa mmoja wa polisi. Mmoja wa walioathirika amebakia hospitali, Muluka alisema. Wakazi wa eneo hilo walisema mgahawa huo unajulikana kwa kuhudumia milo ya nyama ya nguruwe.
Hakuna yeyote aliyedai mara moja kuhusika na mashambulio ya Jumamosi na mamlaka husika hazijasema lolote kuhusu nani anaweza kuhusika na mashambulio hayo.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Hata kanisani watu wachunguzwe ili kuepuka maafa.
Jamani, hiyo inaonesha jeshi letu la Kenya halifanyi kitu, vinginevyo wangepata somo kutokana na milipuko iliyotangulia ya Garisaa na Nairobi. ANEYEPIGWA MARA MOJA, HUONA HAYA MARA YA PILI. Mohammed Noor mkazi wa Isiolo.