Pakistan yajadiliana kuachiwa kwa mateka kutoka kwa maharamia wa Somalia

Machi 30, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kamati ya Pakistani imefikia mwafaka siku ya Alhamisi (tarehe 29 Machi) kuhusu kuwaachia huru mateka waliokamatwa na maharamia wa Somalia miezi 17 iliyopita wakati wa kuteka nyara katika Ghuba ya Aden, viongozi walisema.

Kamati hiyo iliongozwa na viongozi waandamizi wa siasa kutoka Pakistani, walikataa maharamia kulipiwa fidia walioombwa ya dola za kimarekani milioni 10, lakini walikubaliana kuwalipa gharama walizoingia kwa miezi 17 iliyopita, chombo cha habari cha Gulf huko Jamuhuri ya Kiarabu kiliripoti.

Watu 21 waliotekwa walikuwa mabaharia waliokuwa katika meli ya mizigo ya MV Albedo wakati ilipotekwa nyara mwezi Novemba mwaka 2010. Baharia mmoja ambaye ni raia wa India alifariki kwa kipindupindu akiwa kifungoni. Mabaharia wengine walikuwa ni kutoka Pakistan, Srilanka, Bangladesh na Iran.

"Tangu mahakama ya kikabila itoe hukumu dhidi ya uharamia na dhidi ya kulipa fidia yoyote kwa mateka iliwalazimisha kuomba gharama kama uamuzi wa mwisho, na mwisho tuliishia katika malipo ya Dola za Marekani 50 kwa mtu mmoja kwa siku," alisema Gavana Ishratul Ebad Khan wa Jimbo la Sindh la Pakistan. "Kwa kuzingatia takriban watu 100 walikaa katika meli kwa kipindi chote hicho, jumla ya gharama ni Dola za Marekani milioni 2.85."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo