Rais wa Somalia amewataka viongozi wa Kiarabu kusaidia, mafunzo

Machi 30, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliwaomba viongozi katika mkutano wa wakuu wa nchi za kiarabu huko Baghdad Alhamisi (tarehe 29 Machi) kuongeza msaada kwa Somalia.

Ahmed pia alitoa wito kwa wakuu wa nchi za Kiarabu kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Somalia ili kusaidia kurejesha amani na utulivu katika nchi na kuwashinda al-Shabaab, Mtandao wa Habari wa Shabelle wa Somalia uliripoti.

Katika taarifa yake ya kufunga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Kiarabu Nabil al-Arabi alisema ajenda zilikuwa na makubaliano tisa yaliyokubaliwa, ikiwa ni pamoja na iliyokuwa na maelezo ya kina ya jitihada za mapambano ya ugaidi wa kimataifa, Mtandao wa Habari wa Kulmiye wa Somalia uliripoti. Makubaliano pia yalitoa wito kwa suluhisho la amani kwa Syria na Somalia.

Viongozi wa Kiarabu wanasaidia Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia katika utendaji wake, al-Arabi alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo