Makampuni ya bima ya Afrika Mashariki yaomba kanuni za muungano

Machi 25, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wadhibiti wa bima wa Afrika Mashariki walisema katika taarifa kwa Benki ya Dunia kwamba viwango vilivyounganishwa vinahitajika kwa ajili ya ushirikiano wa kikanda na upanuzi wa nje ya mipaka, gazeti la The East African la Kenya liliripoti Jumamosi (tarehe 24 Machi).

Taarifa ya Umoja wa Wasimamizi wa Bima Afrika Mashariki (EAISA) ilipendekeza uanzishwaji wa bodi moja ya usimamizi.

"Sheria zilizopo zinaifanya biashara ya bima kuwa ghali katika nchi hizo," alisema Tom Gichuhi, Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Makampuni ya Bima ya Kenya. "Hadi soko la pamoja litakapoanza kufanya kazi, makampuni ya bima ya Kenya hayatafaidika katika fursa mbalimbali za bima katika soko [la Jumuiya ya Afrika Mashariki]," alisema.

Kwa sasa, kampuni za bima zinalazimishwa kuingiza makampuni mapya badala ya kufungua matawi mapya nje ya mipaka ili kuufanya upanuzi kuwa "suala la gharama", alisema Gichuhi.

Kuoanisha sheria ili kupunguza gharama katika upanuzi wa nje ya mipaka kutaongeza biashara ya bima kupenya katika kanda na kufungua fursa za biashara kwa Afrika Mashariki, gazeti liliripoti.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo