Machi 22, 2012
Kamanda anayemaliza muda wake wa kikosi cha AMISOM Meja Jenerali Fred Mugisha ameshutumu mashambulio ya hivi karibuni ya al-Shabaab jiji la Mogadishu na kuwatuliza Wasomali kuwa usalama unaboreshwa.
“Mashambulio haya ni sehemu ya kampeni zao za kujenga uoga na kuogofya watu,” alisema katika taarifa iliyotolewa Alhamisi (tarehe 22 Machi). “Wasomali wote ni lazima wasimame imara dhidi ya maadui hawa wa amani. Tunawahimiza kutuletea taarifa kuhusu mashambulio na milipuko inayoweza kutokea. Tutasimama nanyie kwa kuwa tunatafuta kujenga njia nzuri ya maisha."
Al-Shabaab wamewaonya raia kuepuka majengo ya serikali na vituo vya AMISOM , kwani bado yatabakia kuwa sehemu zinazolengwa kwa mashambulio, Mtandao wa Habari wa Shabelle wa Somalia uliripoti.
“Tunatuma ujumbe wa onyo kwa wasomali wote kutokuwa karibu na vituo vya jeshi la Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia na vituo vya jeshi la AMISOM kuepuka kupoteza maisha kutokana na mashambulio ya kumwaga damu,” alisema msemaji wa al-Shabaab Shekhe Ali Mohamud Rage.
Mugisha alisema wanamgambo walioshirika na al-Qaeda hawahusiki na ustawi wa raia. “Iwapo wangekuwa wanatafuta kuboresha hali ya watu, wasinge washambulia raia wasio na silaha,” alisema.
Vikosi vya Umoja wa Afrika na vya Somalia vimekuwa vikifanya kazi kwa kushirikiana na raia kuzuia hadi asilimia 70 ya zana za mlipuko zilizochimbiwa katika mji huu, kwa mujibu wa AMISOM.
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Al-Shabaab wamekuwa tishio kubwa sana kwa kutilia maana ni kuwa wanafuata itikadi kali za al-Qaeda. Suluhisho pekee kwa hali ya Somalia ni kuongeza operesheni za kijeshi ili kuwatoa al-Shabaab au njia nyingine ni kuwa na mazungumzo ya amani pamoja na magaidi. Mchakato wa amani unaweza kuchukua muda mrefu lakini hatimaye kutakuwa na amani nchini Somalia.
Al-Shabaab hawawezi kukaribia kuwashinda AMISOM.
Kundi la Alshabab linafanya majuhudi kwa kuingiza vijana kwa shida na kuwapatia masilaha na kuwangiza kwa kundi lao bado waki wadogo kwa umri na wakati zingine kwa nguvu kwa vile tunajua mambo ndani ya Somalia hayazoleki, na kwa kwa bahati mbaya kuna maeneo mengi na vijiji kwa mkono ya Alshabab wakiendelea uhalifu na dhulma zao dhidi ya watu maskini na wale wasiopata hata kitu ya kukula.