Umoja wa nchi za Ulaya (EU) kuongeza misaada kwa Somalia

Machi 20, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Umoja wa nchi za Ulaya utaongeza misaada yake ya kibinadamu na maendeleo ya kisiasa nchini Somalia, Mwakilishi maalumu wa Pembe ya Afrika Alex Rondos aliiambia redio ya RBC ya Somalia katika mahojiano yaliyotangazwa Jumatatu (tarehe 19 Machi).

Rondos alikutana na Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali siku ya Jumapili kujadili hali ya usalama. "Nadhani tumeona hali ya usalama imeanza kubadilika huko Mogadishu na nje ya Mogadishu, maeneo mengi yanaonyesha kuwa polepole kuwa na usalama," alisema Rondos.

Alisema anaona ufuatiliaji katika maendeleo ya kisiasa nchini Somalia na jitihada za kuelekea katika Somalia ya muungano baada ya mamlaka ya Serikali ya Mpito ya Shirikisho mwezi Agosti. Alisema pia kwamba Umoja wa nchi za Ulaya unawajibika na uboreshaji wa hali ya maisha kwa watu waliokosa makazi nchini na kuanzisha njia ya wasomali walio nje kurejea nyumbani.

Umoja wa Nchi za Ulaya umechangia zaidi ya Yuro bilioni 1 kwa Somalia na unataka "kuhimiza kitu chochote ambacho kinaanzisha mfumo wa serikali hapa yaani unaoaminika na Wasomali wote", alisema Rondos

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo