Machi 18, 2012
Siku ya Jumamosi (tarehe 17 Machi) Kenya imetangaza kwamba uchaguzi mkuu ujao utafanyika tarehe 4 Machi, 2013, ikimaliza wiki ya mabishano makali baina ya wanasiasa wapinzani, AFP iliripoti.
"Tunafuata uamuzi wa mahakama ya katiba…ambao unatutaka kufanya uchaguzi siku 60 kuanzia siku muda wa bunge utakapokwisha,”alisema Ahmed Issack Hassan, mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC).
Hata hivyo, mahakama pia ilisema uchaguzi ungeweza kufanyika mapema kama kungekuwa na makubaliano ya maandishi kati ya Raisi Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kuivunja serikali ya mseto.
IEBC ilisema haijapokea uamuzi kuhusu jambo hilo baada ya kukutana na viongozi hao wawili, na hivyo, iliamua kuchukua hatua ya kupanga tarehe.
"Imekuwa dhahiri kwetu kwamba hawakusudii kuvunja mseto….Kuna kutokubaliana miongoni mwao kuhusu ni lini kura inapaswa kupigwa,” Hassan alisema. “Ndiyo maana tulijiamulia wenyewe kupanga tarehe.”
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
WOTE MHESHIMIWA WAZIRI MKUU NA MTUKUFU RAISI NI WASHINDANI WA KISIASA. RAILA NA ODM WANATAKA WAPATE URAISI NA KIBAKI ANATAKA KUHAKIKISHA PNU KINAPATA URAISI. IKIWA WATATEGEMEA TAREHE YA UCHAGUZI, BADO KUTATOKEA MABABAIKO. IEBC LAZIMA IONGOZE NJIA, LAKINI NJIA INGEKUWA IKUBALIANE NA KATIBA MPYA YA KENYA NA IONEKANE NI HAKI NA WAKENYA WALIO WENGI.