Machi 16, 2012
Baraza la Mawaziri la Somalia lilifanya kikao cha dharura Alhamisi (tarehe 15 Machi) baada ya shambulio la bomu la kujitoa muhanga lililoua watu watano katika makazi ya rais, Mtandao wa Habari wa Shabelle wa Somalia uliripoti.
Mkutano huo ambao haukuruhusu waandishi wa habari au umma kuingia uliongozwa na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali, baada ya hapo msemaji wa serikali Abdirahman Omar Osman “Yarisow” alisoma taarifa akibainisha mlipuaji kuwa ni Omar Garweyne, Shirika la habari liliripoti.
Mmoja wa [wafanyakazi] kutoka ofisi ya rais… alimsaidia mlipuaji kufika katika eneo la kasri,” AFP ilimnukuu Yarisow wakati akisema. Mlipuaji alipita vituo vitatu vya ukaguzi, baada ya hapo alilipua fulana yake iliyokuwa na bomu, akijiua mwenyewe na watu wengine watano akiwemo mshirika wake, AFP iliripoti.
Al-Shabaab walidai kuhusika na shambulio hilo na kutoa wito kwa wasomali “kushiriki katika vita dhidi ya makafiri na Serikali iliyoasi dini” msemaji wa al-Shabaab Sheikh Ali Mohamud Gare alisema Jumatano jioni, kwa mujibu wa AFP.
Al-Shabaab wameamua kutumia mbinu za wapiganaji wa msituni baada ya kuondolewa katika ngome zake huko Mogadishu mwezi Agosti.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Somalia ni nchi iliyo na mchanganyiko wa Waafrika, Waislamu na Waarabu, kwa hivyo, utambulisho huu lazima udumishwe na uingiliaji kati wowote, uwe wa kikanda au wa kimataifa, lazima uzingatie muundo huo.