Machi 11, 2012
Mapambano kati ya vikosi vya serikali ya Somalia vikisaidiwa na vikosi vya Ethiopia na wapiganaji wa al-Shabaab karibu na kijiji cha Yurkut cha Somalia Jumamosi (tarehe 10 Machi) yameua wapiganaji wengi wa pande zote, AFP iliripoti.
Afisa anayeiunga mkono serikali Kalif Adan alisema kwamba al-Shabaab waliivamia Yurkut Jumamosi asubuhi. "Wengi wao waliuawa katika mapigano makali. Mapigano sasa yamekwisha na al-Shabaab wamepigwa sana,” aliiambia AFP.
Kamanda wa al-Shabaab Sheikh Mohammad Abu Fatma pia alidai kushinda. “Wapiganaji wa mujahidina waliongoza uvamizi wao muhimu sana wa kijeshi dhidi ya maeneo ya adui huko Yurkut,” alisema.
Vyanzo vya jeshi katika makambi yote vilitoa idadi ya vifo inayotofautiana, lakini vilisisitiza ukali wa mapambano ya saa tatu, kwa mujibu wa AFP.
Yurkut ni sehemu muhimu barabarani inayounganisha mpaka wa Somalia na Ethiopia na Baidoa, iliyokuwa ngome ya al-Shabaab kusini mwa Somalia ambayo vikosi vya Ethiopia na Somalia viliiteka mwezi uliopita.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji