Kikosi cha Kenya kujiunga na AMISOM wiki ijayo

Machi 09, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Askari wa Kenya watajiunga rasmi na kikosi cha Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia wiki ijayo, msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emanuel Chirchir alisema katika Twitter hapo Alhamis (tarehe 8 Machi).

"Kuvaa kofia za kijani ambazo tumezisubiri siku nyingi hatimae kutatokea kwa askari mmoja moja/katika uwanja wa vita wiki ijayo," Chirchir alisema, bila ya kutaja siku hasa. "Tuko imara na AMISOM".

Vikosi vya Kenya, ambavyo vilingia Somalia mwezi Oktoba 2011, litajiunga na majeshi ya Umoja wa Afrika kutoka Uganda, Burundi na Djibouti, chini ya upanuzi wa AMISOM kulikoamuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita. Jeshi la Ulinzi la Kenya lilitangaza wiki iliyopita kuwa Jeshi la Kenya litaendelea nchini angalau mpaka utawala wa AMISOM utakapomalizika mwezi Oktoba mwaka huu.

Chirchir vilevile alisema kuwa vikosi vya Kenya na Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia vilianzisha shambulizi huko Aglibah, kusini mwa Afmadow hapo Alhamis, na kuua wapiganaji sita wa al-Shabaab. Bunduki mbili za AK-47, risasi 200 na mitambo minne ya kurushia mabomu vilikamatwa wakati wa operesheni hiyo, alisema Chirchir.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 7)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo