Ulaya yasimamia juhudi za Putland dhidi ya uharamia, yatoa fedha za ziada kwa AMISOM.

Machi 08, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Ujumbe wa Ulaya uliwasili Puntland Jumatano (tarehe 7 Machi) kutathmini juhudi dhidi ya uharamia katika mkoa huo, mtandao wa Habari wa Shabelle wa Somalia uliripoti.

Wawakilishi thelathini na watatu kutoka Uingereza, Norwe, Denmaki na Uholanzi walitembelea Garowe kuhakiki miradi dhidi ya uharamia inayogharimu mamilioni ya dola inayofadhiliwa na Ulaya, kwa mujibu wa Mkurugenzi anayekabili uharamia wa Puntland Abdirizak Mohamed Ducaysane.

Wakati huohuo, Umoja wa nchi za Ulaya uliahidi kuongeza ugharimiaji kwa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia kwa dola milioni 132, pamoja na kuongeza uwepo wa jeshi lake katika maeneo maji ya Pembe za Afrika. Gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Jumatano. Tangazo hili lilikuja kufuatia mkutano uliofanyika Brussels kati ya Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga na rais wa Baraza la Ulaya Herman Van Rompuy.

Umoja wa Ulaya utaongeza operesheni za jeshi lake la majini katika Pembe ya Afrika hadi 2014, ukipeleka ujumbe wa kusimamia migogoro ya kiraia kujenga uwezo wa mambo ya bahari katika mkoa huo.

“Ni tumaini langu kuwa kwa kuunganisha nguvu tutaweza kuchangia kuongeza usalama nchini Somalia na kurejesha amani na utulivu katika nchi hii,” Van Rompuy alisema. Rais wa Ulaya pia aliishukuru Kenya kwa kuchangia maasikari kwa AMISOM.

Odinga, ambaye aliomba Ulaya na nchi nyingine kuendelea kuwajibika katika kuimarisha Somalia, alisema kuna “mwanga mwishoni mwa shimo refu la chini kwa chini la kutoka sehemu moja kwenda nyingine” kuhusiana na mgogoro wa Somalia, akiwataka kuwekeza kaskazini mwa Kenya pamoja na Somalia.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • hanad yare
    March 23, 2012 @ 01:32:25AM

    Kutokana na shughuli za maharamia nchi nyingi zinaogopa kufanya biashara na nchi ambazo njia zake za baharini zipo karibu na Somalia. Hii ina maanisha kuna ukuaji wa uchumi mdogo kwa sababu pesa nyingi zitatumika kulipia pesa za kukombolea au kutumia vikosi vya kijeshi ili kuongoza bidhaa.

  • Mohamed Salh
    March 9, 2012 @ 11:41:46AM

    Nimevunjwa moyo sana na msaada wa fedha uliopewa Puntland na Somaliland kutoka Jumuiya ya Ulaya. Ningependa kuwashauri wasichukue fedha hizo kwa sababu hazikutolewa kwa nia njema lakini kwa kukidhi maslahi yao ya uchoyo. Wanataka kuchukua mafuta yaliyogunduliwa Somalia kwa msaada wa fedha badala yake.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo