Machi 06, 2012
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesisitiza wajibu wa serikali katika usawa wa jinsia siku ya Jumapili (tarehe 4 Machi) kabla ya mkusanyiko wa kimataifa wa watu wanaopanda Mlima Kilimanjaro kubainisha suala la unyanyasaji dhidi ya wanawake, gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.
"Hatutasita katika jitihada hizi; Niko tayari kufanya kazi na wenzangu katika nchi nyingine kusitawisha chanzo hicho cha unyanyasaji katika bara la Afrika," Kikwete aliwaambia wawakilishi takriban 90 kutoka katika nchi 36 za Afrika, akiongeza kwamba unyanyasaji wa kijinsia unazizuia jamii kuendelea.
Kikwete aliwapongeza viongozi wa wilaya kwa kuungana ili kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia na kurejea itifaki katika Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Haki za Watu kuhusu Haki za Wanawake barani Afrika, unaojulikana vizuri kama Itifaki ya Maputo (Maputo Protocol), ambayo nchi 46 za Umoja wa Afrika zilitia saini na 28 kati yake zilithibitisha rasmi.
"Leo itifaki hiyo inatumika kama nyenzo muhimu kwa ajili ya kuikumbusha serikali iwajibike katika wajibu tulioufanya," Kikwete alisema.
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
Moto kwenye soko kubwa la Garissa uliharibu zaidi ya maduka 100 usiku wa Jumatatu (tarehe 17 Juni...
Waziri wa Umoja wa Kitaifa wa Djibouti Zahra Youssouf Kayad alisaini mikataba ya miradi miwili ye...
Kamati ya bajeti ya Bunge ya Kenya imekataa pendekezo la kununua ofisi mpya kwa aliyekuwa Rais Mw...
Moto ulifanya uharibifu mkubwa katika mji wa Balbala huko Djibouti siku ya Jumapili (tarehe 16 Ju...
Picha ambazo al-Shabaab ilizituma siku za Jumapili (tarehe 16 Juni) kwenye mtandao wa Twitter za ...
Polisi nchini Kenya walimuua mtuhumiwa wa ugaidi, Kassim Omolo Otemo, mjini Mombasa wakati uvamiz...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji