Kenya kufufua kiwanda cha nguo

Machi 02, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Serikali ya Kenya inazindua mpango wa shilingi bilioni 1.8 (Dola za Marekani milioni 22) kufufua tasnia dhaifu ya nguo, ambayo imepata shida kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuenea kwa upatikanaji wa nguo zilizotumika (mitumba), gazeti la Business Daily Africa liliripoti Alhamisi (tarehe 1 Machi).

Fedha ambazo zinatoka katika mkopo wa Benki ya Dunia zitatumika kupanua uzalishaji wa pamba, kuvifanya vinu vya kuchambulia pamba kuwa vya kisasa na kupandisha hadhi tasnia ya nguo, ambayo kwa sasa kinafanya kazi kwa uwezo wa asilimia 30, gazeti liliripoti.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Karanja Kibicho alisema wizara itazindua kempeni ya "Nunua Kenya, Jenga Kenya" ili kupandisha hadhi nguo zinazotengenezwa nchini. " Hii itakatisha tamaa kukua kwa haraka kwa tasnia ya mitumba [nguo zilizotumika], ambayo kimsingi ni kumwaga bidhaa nchini," alisema Kibicho katika uzinduzi wa taasisi ya nguo na ngozi huko Thika.

Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi ya Kenya imepandisha takribani mara mbili ushuru wa forodha wa usafirishaji wa kontena mwezi Desemba, pia iko katika mchakato wa kupandisha mara mbili bei ya nguo zilizotumika (mitumba), kwa mujibu wa chama cha wafanyabiashara cha Gikomba.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • solomon mangira kipkosgei
    June 26, 2012 @ 07:38:10AM

    Ukosefu wa ajira unaoikumba Kenya ni kutokana na kutupa nguo kongwe katika nchi. Tuamke na kukubali kufufua viwanda vyetu kama ambavyo Chuo Kikuu cha Moi kimefanya.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo