Maafisa wawili wauawa baada ya shambulizi la al-Shabaab huko Garbaharey

Machi 02, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wapiganaji wa al-Shabaab walilenga shambulizi katika mji wa Somalia wa kusini-magharibimwa Garbaharey usiku kucha hapo Alhamisi (tarehe 1 Machi) na kuua maafisa waandamizi wawili wa kijeshi na kuwajeruhi wengine kadhaa, Shirika la Habari la BBC liliripoti.

Al-Shabaab walitumia zana nzito, ikiwa ni pamoja na maroketi na magari yenye bunduki, katika jaribio la kuuteka upya mji wa kimkakati, ambao ilikuwa imeushikilia mpaka mwaka jana. Garbaharey sasa unatumiwa na wanajeshi wa Ethiopia na wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) kama kambi ya kuwashambulia al-Shabaab.

Mapigano yaliendelea hadi Ijumaa asubuhi, lakini askari wa Somalia waliukamata mji huo. "Garbaharey bado uko katika udhibiti wetu," alisema mbunge wa eneo hilo Muhammad Sayyid Adan. "Tulipoteza watu wawili katika vita, na majeruhi hawako katika hali mbaya," alisema.

Wapiganaji watano wa al-Shabaab waliuliwa katika mapigano hayo, alisema Jamal Hassan Sarey, mkuu wa vikosi vya TFG huko Garbaharey, kwa mujibu wa Redio ya Somalia Radio Bar-kulan.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo