Nyaya za chini ya ardhi kuimarisha usambazaji wa umeme Kenya

Machi 01, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kampuni ya Umeme ya Serikali ya Kenya itatumia shilingi bilioni 20 (dola za Kimarekani milioni 241) kwa ajili ya mtandao wa nyaya chini ya ardhi ambao ni mzuri kwa mazingira kutoa huduma makini zisizo usumbufu mkubwa, limeripoti gazeti la Business Daily Africa hapo Jumatano (tarehe 29 Februari).

“Mradi huu utamaanisha usambazaji bora na wa kuaminika, unaopunguza makosa na usumbufu katika mfumo wa usambazaji,” alisema Joseph Njoroge, ambaye ni meneja mkurugenzi wa Shirika la Umeme la Kenya.

Laini za umeme za juu ya ardhi sasa zitahamishiwa chini ya ardhi, kwa kuanzia na wilaya za biashara katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu. Hatua hiyo itapunguza kukatika kwa umeme kutokana na sababu za kimazingira na hali mbaya ya hewa, alisema Njoroge.

Nyaya za chini ya ardhi zinachukuliwa kuwa ni salama kwa mazingira kwa sababu zinaepusha matumizi ya nguzo na ukataji wa miti kwa ajili ya kusafisha njia ya laini ya umeme, na pia zinapunguza utoaji wa maeneo ya umeme, limeripoti gazeti hilo.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo