Februari 23, 2012
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inashughulikia mpaka asilimia 40 ya makontena huko Dar es Salaam wakati Huduma za Kimataifa za Makontena Tanzania (TICTS) inafanya ukarabati ili kuboresha ufanisi, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti Alhamisi (tarehe 23 Februari).
"TICTS inakarabati kreni yake ya melini hadi ufukweni. [Kwa vile] kuna kazi ya ujenzi inaendelea, TPA imeingilia kati katika kuziba pengo,” alisema Emmanuel Mallya, mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania.
Wiki iliyopita, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Baharini (SUMATRA) aliwapa TICTS na mawakala wa kupokea na kuhamisha mizigo miezi mitatu kuboresha ufanisi ili kuepusha kuchelewa kwa mizigo. Ikiwa uboreshaji utakuwa hautoshi, mashirika ya usafirishaji ya meli yataruhusiwa kutoza mpaka dola za Kimarekani 250 kwa faini ya chombo kilichochelewa kutolewa.
“Mdau yeyote ambaye atachelewa kuondosha mzigo atachukuliwa kuwa ndiye dhamana,” alisema Meneja wa Masuala ya Umma wa SUMATRA, David Mziray katika barua, akionya kuwa watakuwa dhamana kwa kulipa malipo ya ziada yatakayotozwa.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji