Februari 23, 2012
Uturuki imechangia dola milioni 365 kama fedha taslimu na njia nyingine za msaada kwa Somalia kwa mwaka uliopita, alisema Waziri Mkuu wa Uturuki hapo Jumatano (tarehe 22 Februari).
Uturuki imekuwa ikiongoza jitihada za misaada kwa Somalia, ambapo ukame uliua watoto 29,000 mwaka jana, imesema katika taarifa yake Ofisi ya Mratibu wa Diplomasia ya Umma iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nchi hiyo pia inashiriki katika mkutano wa London kuhusu Somalia ulianza hapo Alhamisi.
Katika habari nyingine, wafanyakazi wa huduma ya maji wa Uturuki wamefungua visima viwili ambavyo vitasambaza huduma hiyo kwa Wasomali 126,000 wanaoishi kwenye kambi za muda mjini Mogadishu, meneja wa mradi Ismail Sevim ameliambia shirika la habari la Uturuki, Anadolu, hapo Alhamisi.
“Watu wanaoishi kwenye kambi hii walilazimika kuchota maji kwenye kisima kilicho umbali wa kilomita mbili,” alisema Mehmet Citil, mratibu wa shirika la misaada la Uturuki nchini Somalia linaloitwa Helping Hand. “Sasa wamefurahi maana wana maji yao wenyewe.”
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji