Februari 23, 2012
Maafisa kutoka nchi 50 na mashirika yalikusanyika London hapo Alhamisi (tarehe 23 Februari) ili kujadili mpango mkuu kwa serikali ya Somalia.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon walikuwa miongoni mwa maafisa waliotaka hatua zichukuliwe kuhusu Somalia, na kutahadharisha kuwa dunia “italipa gharama” kwa kukosa kushughulikia machafuko ya kisiasa, wanamgambo wa Kiislamu na maharamia, AFP liliripoti.
“Matatizo haya ya Somalia hayaiathiri Somalia pekee. Yanatuathiri sote. Ikiwa sote tunakaa pembeni na kuangalia tu, tutalipa gharama kubwa kwa kufanya hivyo," Cameron alisema wakati wa kufungua mkutano. “Ikiwa kila mmoja atashirikiana na wengine kufanya japo kitu kidogo, ninahakika kabisa kuwa Somalia inaweza kutatua matatizo yake na hatimaye kutimiza wajibu wake kama muhusika mkuu ndani ya Afrika na duniani.”
Clinton alisema Marekani itashinikiza juu ya vikwazo, ikiwa ni pamoja na marufuku ya kusafiri na kuzuia mali kwa wale ambao “wanaweka vikwazo” kwa ajili ya maendeleo ya serikali ya mpito, utawala ambao unamaliza muda wake mwezi wa Agosti.
“Kwa miongo mingi, dunia imekuwa ikishughulikia katika kile ambacho yungeweza kukizuia kisitokee Somalia – iwe ni mgogoro wake, njaa au majanga mengine. Sasa tunakabiliwa na kile ambacho tunaweza kukijenga. Fursa hii ni ya kweli,” Clinton alisema.
Vilevile aliomba ziada ya dola za Kimarekani milioni 64 kwa msaada wa kibinadamu katika eneo hilo ili kusaidia kuboresha maisha ya Wasomali wa kawaida, waliokumbwa na njaa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda wa miaki 21 iliyopita.
Ban yeye aliutaka ulimwengu kujenga juu ya maendeleo ya hivi karibuni baada ya Umoja wa Mataifa kukubali kukiinua kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika katika nchi kwa kupeleka zaidi ya wanajeshi 17,000, na baada ya wanamgambo wa al-Shabaab kutolewa kutoka mji muhimu hapo Jumatano.
“Tumefungua nafasi kwa ajili ya amani na utulivu Somalia. Ni nafasi ndogo, lakini inawakilisha fursa ambayo hatuwezi kuifanya tuipoteze,” Ban alisema.
Huko Mogadishu, wakazi walipeperusha bendera za Uingereza zilizotengenezwa kwa mkono ili kuonesha kuunga mkono kwa mkutano huo, kwa mujibu wa AFP, hata baada ya milipuko miwili kuripotiwa huko Baidoa, mji ambao ulitekwa upya kutoka kwa al-Shabaab hapo Jumatano.
Mkutano huo unawaleta pamoja maafisa kutoka nchi 40, ikiwa ni pamoja na viongozi wa Ethiopia, Uganda na Kenya, pamoja na Umoja wa Afrika na Umoja wa Kiarabu.
Cameron alisema kuwa dunia sasa ina kazi tatu kubwa: kuisaidia Somalia kuimarisha usalama, kufikisha misaada ya kibinadamu katika sehemu inayohitajika, na kuzisaidia juhudi za Somalia katika kujenga serikali wakilishi.
Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali alisema katika kipindi cha kuelekea mkutano, kuwa nchi yake ilikuwa “inaelekea katika kipindi enzi ya amani, cha amani, utulivu na hali ya kawaida”.
Raisi wa Somalia, maraisi wa majimbo yenye utawala wa ndani ya Puntland na Galmudug, kamanda wa wanamgambo dhidi ya al-Shabaab, Ahlu Sunna wal Jamaa walitia saini makubaliano yaliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa hapo Jumamosi, makubaliano yanayoelezea muundo wa serikali mpya itakauochukua nafasi ya serikali ya mpito hapo mwezi wa Agosti.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Lengo lililotangazwa la mkutano wa London ni kukubali hatua za kutekeleza na kuunga mkono mchakato mpya wa kisiasa pamoja na kutoa msaada kwa maeneo mengi ya Somalia na kutoa fedha kwa misheni ya Umoja wa Afrika, pia kuchukua hatua za kufaa za kupambana na uharamia na ugaidi na kuongeza uratibu wa misaada ya kibinadamu. Lakini hii imeonekana wazi baada ya kuibuka kwa mgogoro juu ya utajiri wa mafuta na uranium vilivyogundulika Somalia hivi karibuni. Maneno haya yanaonesha kile kilicho nyuma ya ulazimishaji na upelekaji wa majeshi mengi zaidi ya kigeni nchini Somalia, uzuwiaji wa matumizi ya bahari ya Somalia na nyenzo za majini na kuendelea kwa operesheni ya uvuvi haramu na utupaji wa takataka zenye sumu. Somalia imesambaratika na kuangukia katika mzozo kutokana na ushindani juu ya malighafi na uongozi.
Hali katika Somalia ni mbaya sana. Kuna watu wapatao milioni 9 wenye njaa ambao hawamudu hata chakula chao. Watu wanaishi katika hali za kukatisha tamaa licha ya kuwepo malighafi tele zinazoweza kuwalisha. Wanamgambo wenye siasa kali waliwalazimisha watu kwenda vitani, vita ambavyo hakuna yoyote nchini anayejua vitakwisha lini. Upatikana kwa maji safi ya kunywa na dawa ni mchache. Iko haja ya kuja kuwaokoa watu wa Somalia kutokana na matatizo hayo. Hali sasa imedhibitika na kunahitajika vitu vichache kutoka kwa mashirika ya kibinadamu. Onyo langu ni kuwa iko haja ya kumaliza utapiamlo, ukame na vurugu.