Bendera nyeusi ya al-Shabaab yaondolewa kutoka katikati ya mji wa Baidoa

Februari 23, 2012

  • 15 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali alithibitisha hapo Jumatano (tarehe 22 Februari) kwamba vikosi vya Ethiopia na Somalia viliukamata mji wa kimkakati wa Baidoa kutoka kwa al-Shabaab.

  • Mtu akipanda juu ya jingo la chuo kikuu cha Somalia ili kuondosha bendera ya al-Shabaab katikati ya mji wa Baidoa hapo tarehe 23 Februari. [Na AFP PHOTO/Stringer]

    Mtu akipanda juu ya jingo la chuo kikuu cha Somalia ili kuondosha bendera ya al-Shabaab katikati ya mji wa Baidoa hapo tarehe 23 Februari. [Na AFP PHOTO/Stringer]

“Moja ya miji muhimu kusini magharibi ya Somalia, Baidoa, ndio kwanza umekamatwa kutoka al-Shabaab,” Ali aliwaambia waandishi wa habari huko London, siku moja kabla ya mkutano mkuu wa kimataifa kuhusu Somalia.

Vikosi vya Somalia na Ethiopia viliripotiwa kuingia Baidoa bila ya mgogoro, kwa vile al-Shabaab tayari walikwishakimbia.

Bendera nyeusi ya al-Shabaab iliondolewa kutoka mlingoti wa bendera katikati ya mji hapo Alhamisi asubuhi na maafisa wa serikali ya Somalia waliapa kuendelea kupambana na wapiganaji wa al-Shabaab.

"Mji ni kimya sana asubuhi hii, na watu wanajisikia huru kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu,” alisema Gavana Abdifatah Mohamed Ibrahim wa eneo la Bay, mji ambao unaijumuisha Baidoa.

Masaa kadhaa baada ya mji kukombolewa kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab wanaoshirikiana na al-Qaeda, milipuko miwili mikubwa iliutikisa mji wa Baidoa Jumatano jioni. Al-Shabaab walidai kuhusika kwa mashambulizi hayo, wakisema kuwa walisababisha uharibifu mkubwa kwa vikosi vinavyoiunga mkono serikali. Lakini madai yao hayakuweza kuthibitishwa.

Msemaji wa kikundi cha wanamgambo, Sheikh Abdulaziz Abu Musab, alisema milipuko ilivilenga vikosi vya Ethiopia na Somalia wakati vikiingia sehemu iliyoachwa na wapiganaji wa al-Shabaab, huku wakiapa kuwa kuendeleza mgogoro “mpaka Uislamu uwe ndio kanuni pekee inayotawala nchi”.

Mkazi mmoja, Warsame Adan, aliliambia Shirika la Habari la AFP kuwa kiwanda cha eneo hilo kililengwa katika mmoja wa milipuko baada ya vikosi vya Ethiopia vilipoukamata mji, aliliambia. “Hatujui kama kuna waathirika wowote, kwa vile hatukuweza kutoka nje usiku kwa sababu kulikuwa na amri ya kutotembea,” alisema.

Baidoa ilikuwa mojawapo ya ngome kuu ya al-Shabaab, na kukamatwa kwake kunawaacha wapiganaji wa kikundi hicho katikati ya mji kuwa wametengwa, AFP iliripoti. Wanamgambo bado wanadhibiti sehemu kubwa za kusini ya Somalia, ambako wanakabiliwa na upinzani wa nchi kavu na angani kutoka Jeshi la Ulinzi la Kenya.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 80)

Dislike_icon(18)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Dayow
    October 5, 2012 @ 10:35:29AM

    Wapendwa nyote, al-Shabaab haina uhusiano wowote na Uislamu au Mujahidina kama wanavyodai. BALI ni wahuni tu waliochanganyikiwa wanaohitaji kusafishwa nje ya Somalia na taifa kubwa la Somalia litakuwa na amani na tutarejesha utukufu wake!

  • Abdulswamad
    May 6, 2012 @ 12:51:26PM

    Nyinyi makafiri wa kiamerika kwa nini munawatesa waislamu waacheni waanzishe hizo dola zao za kiisalamu ,mbona mnapenda kuwaonea waislam ,lakini kwa uwezo wake Allah nyinyi mtashindwa na dola la kiislam litatawala ulimwengu mzima, kila inchi ambayo ina waislaam nyinyi lazima mtazipiga, tumeshakujuweni kwamba nyinyi mnachuki na uislaam basi nasisi tunazidi kukuchukieni na tutapambana na nyinyi.

  • ٍسايمونٍ
    March 18, 2012 @ 08:31:01PM

    Amani iwe juu yenu! Sijui niseme nini, lakini ulimwengu mzima unaiangalia Somalia kama nchi imara, licha hali zake mbaya. Somalia ni nchi pekee ambayo imewaogopesha Marekani. Walipelekwa Somalia na hawakurejea tena. Ama kuhusu suala hili, natumai kuwa mujahidina wataungana na kwamba malengo yao ni kujikomboa na kufanya upatanishi na mtume wetu. Uislamu ni dini ya upendo na utulivu, na amani haiji isipokuwa kwa upanga na nguvu. Sio kama Mayahudi wanavyodai, kuwa amani hupatikana kwa kuwadhalilisha Waislamu na kuwaua kama kondoo nchini Pelestina kila siku. Waarabu bado wana matumaini kuwa Israeli itawapa amani! Ni kichekesho! Waarabu wanaishi katika nchi kubwa kubwa na wana nguvu! Kwa bahati mbaya, wanawaomba Israeli wawape uhuru!

  • Muna
    March 15, 2012 @ 07:26:50AM

    Wanatoka timu moja Al-Qaeda na al-Shabaab si Waislamu, wangekuwa Waislamu katu wasingefanya yasiyofanywa na Waislamu au kuua kila mtu bila ya sababu.

  • neehaa
    March 14, 2012 @ 08:17:45AM

    AL-SHABAAB ni kizuri sana

  • Ali
    March 9, 2012 @ 09:48:38AM

    Wale ambao siku zote wanafanya uhalifu dhidi ya watu wasio na hatia hawawezi kuwakilisha dini ya Kiislamu.

  • kenneth kiruai
    March 4, 2012 @ 08:09:21AM

    Wauwaji hawa wapigwe vibaya sana kiasi wasiishi kuja kujuta. Walengeni viongozi na makamanda wao. Waache wauliwe na kuzikwa kama Osama. Ninaunga mkono vita hivi.

  • paul
    March 2, 2012 @ 11:49:19AM

    Wacha mtu yeyote mwenye akili kuwapiga wahuni hawa kwa njia yoyote inayowezekana. Nina hakika watu wa Somalia watafaidi uhuru wa kweli wakati serikali yao itakapoidhibiti nchi yote.

  • ogeto[kenyan]
    February 28, 2012 @ 09:04:40AM

    NDIO, wanastahiki kufedheheshwa kwa sababu watu wanahitaji kuongoza maisha bila ya kumwaga damu na kuepuka kulia dhidi ya watu wanaovuna kile wasichokipanda. Hongera, hongera watu wetu.

  • Kiplangat joe
    February 28, 2012 @ 05:50:37AM

    Watu wanaopigana kwa jina la Mungu lazima wathamini maisha ya watoto wasio hatia na wanawake na hivi sivyo na al-Shabaab.

  • JAMES WASIKE
    February 27, 2012 @ 05:27:32AM

    Al-Shabaab ni watu wa mzaha tu wanaotaka kutumia vibaya jina la dini. Vikosi vya ulinzi vya Kenya na Ethiopia pamoja na vikosi vya Somalia endeleeni kuwasha moto kwa kuhakikisha kuwa hakuwi na mabaki ya al-Shabaab yoyote hai ndani ya Somalia.

  • masoudjongo
    February 27, 2012 @ 03:38:09AM

    Sisi kama Waislamu hatuna budi kuwaunga mkono al-Shabaab kwa sababu wanapigana kwa ajili ya Uislamu na kwa Mapenzi ya Mungu watashinda.

  • Abdalle
    February 26, 2012 @ 02:35:53AM

    Al-Shabaab na al-Qaeda wanafuata kwa pamoja itikadi zifuatazo: matumizi yao ya nguvu, kueneza propaganda kwa kutumia jina la Sharia ya Kiislamu katika maeneo yao wanayoyalenga, kumbandika mtu jina yeyote ambaye anapinga itikadi zao kuwa ni adui wa Uislamu; kuapa kuwa watammaliza yeyote, au kuangamiza uwepo wa kikundi chochote kinachowapinga. Wao ndio adui wa Uislamu. Matumizi ya vitisho na nguvu ili kupata maslahi yao vilevile kunatumiwa na wote, al-Shabaab na al-Qaeda. Vilevile wanatabia ya kuchukua dhamana ya kuhusika na chochote kinachotokea hata kama hawahusiki. Kwa sababu hii, vikundi vyote viwili lazima viangamizwe kama kilivyoangamizwa kikundi cha Tamil kilichokuwa kinajulikana ka “LTTE” na ulimwengu wote lazima upinge vikundi hivi visivyo vya kistaarabu!

  • Callisto Onyango
    February 24, 2012 @ 12:28:18PM

    Tangu lini jumuiya yoyote ya kidini iliandikisha watoto ili wapigane? Watoto walipaswa walindwe kwa sababu hawaelewi athari za vita. Uislamu hauna tofauti.

  • abdiaziiz aden isxaaq
    February 24, 2012 @ 03:58:24AM

    Amani iwe juu yenu, kwanza kabla ya yote, ndugu zangu mnatarajiwa mukae vyema na Waislamu wa Somalia.[KUTENDEANA MEMA] [NA KUWASHUGHULIKIA VIBAYA WALE WASIOAMINI], kwa hivyo, ndugu zangu ikiwa mtashindwa kuwa na ushawishi kwa watu wenu hakuna mtu atakayewaunga mkono. Kwa hivyo ningewataka kuweka bunduki zenu chini kwa wakati huu na kuwa raia wa kawaida wa Somalia. Muanze tu kupigana ikiwa watakuja na kitu ambacho ni dhidi ya mafunzo ya Kiislamu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo