Umoja wa Mataifa: Njaa imeisha nchini Somalia

Februari 03, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Uchambuzi wa Lishe cha Usalama wa Chakula nchini Somalia kilisema Ijumaa (tarehe 3 Febuari) kuwa njaa nchini Somalia imekwisha, lakini karibu moja ya tatu ya watu bado wanahitaji msaada wa dharura.

“Muunganiko wa kuongezeka sana kwa msaada wa kibinadamu na mavuno yasiyo ya kawaida vimesaidia kuboresha hali ya kibinadamu,” shirika hilo lilisema. Shebelle ya katikati, Afgoye na makambi ya watu wasio na makazi mjini Mogadishu ndizo zilizokuwa kanda za mwisho zenye njaa nchini Somalia, lakini "kwa sasa wameboresha kiwango cha dharura”.

“Mafanikio hayo si imara na linaweza kurudiwa pasipo msaada endelevu,” alisema Mark Bowden Mratibu wa Ubinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia.

Shirika hilo lilisema kuwa watu milioni 2.34 wamebakia katika migogoro, hususani katika mikoa ya kusini ambapo ufikaji umeendelea kuwa na mipaka kutokana na al-Shabaab kudhibiti eneo hilo.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo