Walimu wa Tanzania wasitisha mgomo

Januari 06, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Chama cha walimu Tanzania (TTU) kimefuta mgomo wake Jumatano (tarehe 4 Januari) baada ya Serikali kulipa malimbikizo ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 14, rais wa chama hicho aliwaambia waandishi wa habari.

Chama kimepokea taarifa za uhakika wa malipo ya fedha na kusambazwa kwa marupurupu ya walimu yasiyohusiana na mshahara kupitia Halmashauri zao za Wilaya na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ifikapo tarehe 15 Januari, alisema rais wa TTU Gratian Mukoba.

Mukoba alisema "mtazamo chanya" wa serikali umemaanisha waalimu wanapaswa kuwa madarasani ifikapo Jumatatu, gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.

Aidha, TTU kilimwomba Rais Jakaya Kikwete kujadiliana na chama kuhusu mchakato wa malipo ili kuhakikisha kwamba hakuna makosa yoyote yatakayotokea, Mukoba alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo